The House of Favourite Newspapers

Ishu ya Yanga Kwenda FIFA Kudai Pointi

0

INADAIWA kuwa uongozi wa Klabu ya Yanga umeliandikia barua Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), kudai ushindi wa mchezo dhidi ya Simba uliopangwa kuchezwa Mei 8, mwaka huu, ambao uliahirishwa kufuatia mkanganyiko wa mabadiliko ya muda wa kuanza kwa mchezo huo.

 

Mchezo huo wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara uliahirishwa na Bodi ya Ligi kwa madai ya kupewa maelekezo ya mabadiliko ya muda wa kuanza mchezo kutoka saa 11:00 jioni hadi saa 1:00 usiku kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Baada ya taarifa hiyo, Yanga walitoa taarifa wakidai kwamba mabadiliko hayo ni kinyume na kanuni hivyo wakapeleka timu kwa muda wa awali ambao uliopangwa, na kweli wakafanya hivyo lakini Simba wakafuatisha taarifa ya mabadiliko iliyotolewa na Bodi ya Ligi.

 

Kwa mujibu wa mtoa taarifa wa kuaminika kutoka ndani ya Simba aliliambia Championi Jumatano kuwa: “Kuna taarifa ambazo binafsi zimenifikia kuwa uongozi wa Yanga bado haujafikia muafaka kuhusiana na mchezo dhidi yetu wa Julai 3, na kuna uwezekano wa wa kutoleta timu uwanjani kwa kuwa wameandika barua kwa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), kudai matokeo ya ushindi katika mchezo uliopangwa kufanyika Mei 8, mwaka huu.

 

“Lakini kwetu tunaamini Julai 3, tuna mchezo dhidi ya Yanga na tutaendelea kujiandaa na mchezo huo, kwa kuwa kilichotokea Mei 8, kiko wazi kwa pande zote mbili kuwa lilikuwa ni jambo lililo nje ya uwezo wetu.

 

Alipotafutwa na gazeti hili ili kuzungumzia sakata hilo, Ofisa Habari wa Klabu ya Yanga, Hassan Bumbuli alisema: “Kwa sasa niko na majukumu mengi ya kikazi, hivyo siwezi kuongea lolote kuhusiana na hilo naomba unitafute muda mwingine.”

 

Leave A Reply