#GlobalMusic: Isikilize ‘Fool For You’ Ngoma Mpya Ya Wizkid Iliyovuja – (Audio)

Baada ya ku-sign dili nono na SONY mkali wa muziki kutoka Nigeria Wizkid  amerudi na nyingine mpya.

Mwanzoni mwa mwaka huu Wizkid ali-tweet na kuwaambia mashabiki wake wajiandae kwani mwaka 2017 utakuwa mwaka atakaoongoza kwa kutoa album nyingi, akiahidi kutoa album 4.

Kuelekea safari hiyo, siku ya jumanne baadhi ya kazi za mkali huyo zilianza kuvuja mtandaoni na kuleta shauku kubwa kwa mashabiki waliofanikiwa kuupata wimbo wake mpya uitwayo ‘Fool For You’.

Hii itakuwa ni mara ya pili kwa mwaka huu kwa kazi za Wizkid kuvuja bila ridhaa yake na kwa mujibu wa baadhi ya ripoti zinazotolewa inasemekana hata SONY wenyewe hawajafurahishwa na kitendo hicho huku Wizkid nae akisikitishwa na kitendo hicho kumtokea mara kwa mara.

Ngoma yenyewe ipo hapa chini, isikilize alafu niambie kwenye comments unaionaje.

 Wizkid – ‘Fool For You‘. 

Imeandikwa Na: Sandra Brown

Subscribe kwenye YouTube Chanel yetu ya Global TV Online ili zote kali zinazotufikia iwe ni siasa, michezo, comedy, burudani, stori za mastaamuziki na nyingine zikufikie kwa wakati.

Loading...

Toa comment