Israel yabomoa makazi ‘haramu’ yaliyojengwa Palestina

Israel imeanza kubomoa makazi kadhaa ya Wapalestina ambayo inasema yalijengwa kinyume cha sheria, karibu sana na eneo linalougawa Ukingo wa Magharibi.

Maofisa wa usalama wameinga katika eneo la Sur Baher, katika eneo la Jerusalem mashariki, kuzibomoa nyumba hizo zinazosemekana kuwahifadhi watu 17. Wakazi wa sehemu hiyo wanasema walipewa vibali vya kuwaruhusu kujenga kutoka Mamlaka ya Palestina, na wameishutumu Israel kwa kujaribu kuinyakua ardhi hiyo.

Mahakama ya juu zaidi ya Israel iliamua kwamba walikiuka marufuku ya kutojenga katika eneo hilo. Israel ililiweka chini yake eneo hilo la  mnamo 1967 katika vita vya Mashariki ya Kati na baadaye kulitenga eneo la Jerusalem Mashariki.  Kwa mujibu wa sheria za kimataifa, maeneo yote yanatazamwa kuwa makazi yaliyokaliwa, licha ya kwamba Israel inapinga  jambo  hilo.

Kiasi cha maofisa 700 wa polisi wa Israeli na wanajeshi 200 walihusika katika operesheni hiyo leo katika kijiji cha Wadi Hummus, ukingoni mwa Sur Baher. Waliingia wakiwa wamejihami kwa matingatinga yaliyoanza kubomoa majengo hayo kumi  ambayo Umoja wa Mataifa ulisema yalikuwa yamelengwa kubomolewa.

Raia tisa wa Palestina walioathirika ni wakimbizi wakiwemo watoto,  kwa mujibu wa Umoja wa mataifa. Wengine 350 waliokuwa na makazi katika eneo hilo ambayo hayana watu au yalikuwa bado yanajengwa. Mmoja wa wakazi hao, Ismail Abadiyeh, ameliambia shirika la AFP kuwa familia yake ‘itasalia barabarani’.

Waziri mkuu katika Mamlaka ya Palestina, Mohammad Shtayyeh, amesema raia wa Palestina watalalamika katika mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai (ICC) kuhusu ‘uchokozi huo mkubwa’.

“Huu ni muendelezo wa kuwatoa watu kwa lazima katika makazi yao na ardhi zao – uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binaadamu,” ameongeza

Lakini waziri wa usalama wa wananchi,  Gilad Erdan,  amesema mahakama ya juu zaidi ya Israel “iliamua pasi na shaka kwamba majengo hayo yalijengwa kinyume cha sheria karibu na ua wa usalama na kutishia maisha ya raia na vikosi vya usalama”.

Mratibu wa misaada ya kibinadamu katika Umoja wa Mataifa, Jamie McGoldrick,  aliiomba Israel wiki iliyopita kufutilia mbali ubomoaji huo na badala yake iidhinishe “sera za usawa za upangaji” kwa Wapalestina.

 


Loading...

Toa comment