Israel imesitisha usambazaji wa umeme katika Ukanda wa Gaza katika juhudi za kushinikiza Hamas kukubali kuongezwa muda wa awamu ya kwanza ya makubaliano ya kusitisha mapigano.
Makubaliano hayo yalifikia ukomo mwishoni mwa wiki iliyopita, na hatua ya Israel inaweza kuwa na athari kubwa, hasa kwa mitambo ya kusafisha maji ya chumvi ambayo hutegemea umeme kutoka Israel.
Ukanda wa Gaza umeharibiwa vibaya kutokana na mashambulizi ya kijeshi ya Israel tangu Oktoba 2023. Baadhi ya wasambazaji wa nishati wamekuwa wakitumia majenereta na nguvu ya jua kama vyanzo mbadala vya umeme.
Hamas imeitaka awamu ya pili ya makubaliano ya kusitisha mapigano ianze mara moja ili kufanikisha suluhisho la kudumu kwa mzozo huo.