The House of Favourite Newspapers

Israeli Yadai Kumuua Kiongozi Mwingine wa Hezbollah, Nabil Kaouk

0
Kiongozi mwingine mkuu wa Hezbollah, Nabil Kaouk

Jeshi la Israeli kupitia ukurasa wake kwene mtandao wa kijamii wa X (Twitter), limesema kwamba limemuua kiongozi mwingine mkuu wa Hezbollah, Nabil Kaouk, mmoja wa viongozi wachache wakuu waliobaki wa kundi hilo.

Jeshi la Israeli limesema aliuawa katika shambulio la anga hapo jana, Jumamosi, Septemba 28, 2024.

Kaouk alikuwa mwanachama mkongwe wa Hezbollah tangu miaka ya 1980 na hapo awali aliwahi kuwa kamanda wa kijeshi wa Hezbollah Kusini mwa Lebanon ambapo mpaka anauawa, alikuwa Naibu Mkuu wa Baraza Kuu la Hezbollah.

Marekani ilitangaza vikwazo dhidi yake mnamo mwaka wa 2020.

Kaouk alikuwa akitajwa kuwa miongoni mwa ambao wangerithi nafasi ya Hassan Nasrallah, kiongozi wa Hezbollah aliyeuawa na shambulio la anga la Israeli, Beirut siku ya Ijumaa, kama mkuu wa Hezbollah.

Kufuatia kifo chake, chaguzi za nani atakayeongoza kundi hilo kwa sasa zinazidi kupungua, huku wachambuzi wakipendekeza kuwa Hashim Safieddine, Mkuu wa Baraza la Utendaji la Hezbollah, ndiye chaguo linalopewa kipaumbele.

Naeem Qassem, Naibu Katibu Mkuu wa shirika hilo, pia anaripotiwa kuwa miongoni mwa wanaoweza kushika nafasi hiyo.

Kifo cha Kaouk ni pigo zaidi kwa uongozi wa Hezbollah, ambao tayari umeathirika sana kutokana na kampeni ya mauaji ya kimkakati ya Israeli.

NDEGE ya WAZIRI MKUU wa ISRAEL YANUSURIKA KUTUNGULIWA na WAASI wa HOUTHI WAKITAKA KULIPIZA KISASI…

Leave A Reply