testiingg
The House of Favourite Newspapers

Italia na Tanzania Zafanya Jukwaa la Biashara na Uwekezaji

0
Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Othman Masoud akiongea na wadau wa Biashara na Uwekezaji

KATIKA Jukwaa la Biashara na Uwekezaji kati ya Italia na Tanzania lililofanyika leo Zanzibar ambapo Mgeni Rasmi Alikuwa Makamo wa Kwanza wa Rais Othman Masoud.

 

Jukwaa hilo pia lilihudhuriwa na Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Zanzibar Uwekezaji, Soraga na Mabalozi wa Tanzania nchini Italia Mahmoud Thabit Kombo na Balozi wa Italia nchini Tanzania Marco Lombardi.

 

Pia walikuwepo Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali na Wafanya Biashara wa Zanzibar na zaidi ya Wafanyabiashara 100 kutoka nchini Italia.

Wadau wa Biashara na Uwekezaji wakisikiliza hotuba ya Makamu wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Othman Masoud

Jukwaa hilo lilifanikiwa kwa kiasi kikubwa pakiwepo na mikataba mitano iliyosainiwa ya mashirikiano kati ya Kampuni kutoka Italia na Zanzibar.

 

Kesho, Jukwaa kama hilo litafanyika Jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere Convention Centre kuanzia saa tatu kamili asubuhi ambapo mgeni Rasmi katika Uzinduzi huo anatarajiwa kuwa Mhe. Kijaji, Waziri wa Uwekezaji.

Leave A Reply