Italian Trade Agency (ITA) Yazindua Mafunzo ya Lab Innova kwa Tanzania

Italian Trade Agency(ITA), ni taasisi ya serikali inayotangaza fursa za uwekezaji kimataifa hususani Italia na kuvutia uwekezaji wa kigeni nchini Italia, kwa kushirikiana na Wizaraya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ya Italia, imezindua kwa mara ya kwanza nchini Tanzania mafunzo ya Lab Innova – “Toleo la Luca Attanasio”, ambayo yamefanyika kuanzia tarehe 3 hadi 7 Februari 2025 katika ukumbi wa Delta Hotel by Marriott jijini Dar es Salaam.
Lab Innova Tanzania – “Toleo la Luca Attanasio” ni mafunzo ya hali ya juu katika nyanja za kiufundi na usimamizi wa biashara, yaliyoanzishwa kwa lengo la kusaidia maendeleo na upanuzi wa biashara za Kiafrika katika sekta ya kilimo-biashara.

Mafunzo haya yamehusisha vipindi vya nadharia, kazi za vikundi, pamoja na uzoefu kutoka kwa wataalamu wasekta, ili kuwawezesha washiriki kuboresha mbinu zao za kilimo kwa kutumia teknolojia na zana za kisasa.
Kupitia mafunzo haya, washiriki 42 waliobobea katika sekta ya kilimo-biashara nchini Tanzania walipata mafunzo ya kina kuhusu biashara ya kimataifa, viwango vya ubora vyaUlaya, uendelevu wa mnyororo wa thamani, matumizi ya teknolojia ya kisasa ya kilimo, pamoja na mbinu bora za kushirikiana na mifumo ya kiuchumi ya Italia.

Mafunzo haya yameimarisha fursa za biashara, uwekezaji na ushirikiano katiya Tanzania na Italia. Aidha, washiriki 8 wa Lab Innova watachaguliwa na kudhaminiwa kushiriki katika ziara maalum ya mafunzo ya siku tano itakayojumuisha kutembelea maonyesho, viwanda vya kilimo, na mikutano ya kibiashara (B2B) katika Maonyesho ya MACFRUT 2025 mjini Rimini, Italia.
Hafla ya kufunga rasmi mafunzo ya Lab Innova kwa Tanzania imehitimishwa na Balozi wa Italia nchini Tanzania, Mhe. Giuseppe Sean Coppola, Mkurugenzi wa Ofisiya ICE Nairobi, Bw. Giuseppe Manenti, Mkurugenzi wa Baraza la Afrika Tanzania, Bw. Timoth Mmbaga, ambaye ni mshirika wa ndani wa mpango huu, Mkuu wa Kitengo cha Kilimo-Biashara wa CRDB Bank PLC, Bw. Margesi Shabaan, pamojanaMenejaMwandamiziwaKitengo cha Kilimo-Biashara cha Rejarejawa CRDB Bank PLC, Bi. Jane Christopher.
Nchi ya Tanzania, hivi karibuni imetangazwa kuwa moja kati ya nchi ambazo iko kipaumbele katika Mpango wa Mattei, ina nafasi muhimu katika sekta ya kilimo na imepiga hatua kubwa katika maendeleo ya sekta hiyo katika kipindi cha miongo kadhaa iliyopita.
Kwa sasa, Tanzania imejielekeza katika matumizi ya teknolojia ya kisasa na uongezaji thamani katika kilimo, huku ikihamasisha biashara na uwekezaji katika viwanda vy akilimo.
Mafunzo haya ya Lab Innova kwa Afrika pia yanakuja katika kipindi muafaka kuelekea Jukwaa la Biashara la Tanzania, ambalo litafanyika tarehe 11 na 12 Februari 2025 jijini Dar es Salaam. Tukio hili litakuwa jukwaa muhimu kwa zaidi ya kampuni 51 kutoka Italia kushiriki na kujadili fursa za biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Italia, hasa katika sekta za Teknolojia ya Kilimo (Agro-Tech), Uchumi wa Bluu, Uchumi wa Kijani, Miundombinu Endelevu, Afya na Madawa.