Kartra

Italy Yaitungua Spain na Kutinga Fainali ya Euro 2020

Timu ya Taifa ya Italia imefanikiwa kutinga Fainali ya michuano ya Euro 2020 baada ya kuiondosha Hispania kwa mikwaju ya penati 4-2 kufuatia kutoshana nguvu katika dakika 120 za mchezo wa nusu Fainali uliopigwa jana usiku, Julai 6, 2021 katika dimba la Wembley jijini London nchini Uingereza.

Hispania walionekana ku-dominate mchezo kuanzia kipindi cha kwanza mpaka mwisho wa game lakini kwa nyakati tofauti timu zote mbili zilishambuliana ambapo mpaka dakika 45 za kwanza zinatamatika timu zote zilikuwa hazijafungana.

Italia walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Federico Chiesa dakika ya 60 huku Hispania wakisawadhisha kunako dakika ya 80 ya mchezo kupitia kwa Alvaro Morata ambapo mpaka dakika 90 zinatamatika timu zote zilikuwa sare ya bao 1-1.

Dakika 30 ziliongezwa lakini mpaka zinatamatika timu zote zilikuwa sare ya bao 1-1 ndipo matuta yakatengwa kuamua mshindi.

Baada ya Italy kuibuka washindi sasa watakutana katika fainali ya Euro 2020 na mshindi atakayepatikana katika mchezo wa nusu fainali ya pili kati ya Denmark na Uingereza itakayopigwa leo Julai 7, 2021 saa 4:00 usiku katika Dimba hilo hilo la Wembley.


Toa comment