The House of Favourite Newspapers

ITM Tanzania Yaadhimisha Miaka 5 Wakati Serikali Ikiahidi Kuwezesha Sekta Ya Rasilimali Watu

0
Meneja wa Kampuni ya ITM Tanzania, Adelaida Kwai akizungumza na wageni waalikwa kwenye hafla ya kusherehekea maadhimisho ya miaka mitano ya kampuni ya ITM Tanzania iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Dar es Salaam. Ijumaa Mei 19, 2023. Katika jitihada za kuibua na kuhakikisha ukuaji wa vipaji vya ndani katika soko la ajira linalohitajika kila mara, serikali ya Tanzania itaendelea kujitahidi kuweka sera na kanuni zitakazotoa mwanya wa ukuaji wa sekta hiyo, ikiwa ni pamoja na kukuza ushirikiano wa kimkakati na wataalam katika kuhifadhi vipaji, upatikanaji na mafunzo ya kitaaluma.

Uongozi wa Kampuni ya ITM Tanzania wakikata keki wakati wa hafla ya maadhimisho hayo.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala (DAS), Charangwa Selemani aliyasema hayo mwishoni mwa wiki, ambapo alibainisha kuwa, ili kuhakikisha ukuaji endelevu wa soko la ajira nchini, sekta hiyo inahitaji juhudi za mashirikiano kutoka serikalini na sekta binafsi.

DAS alikuwa akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla ya kuadhimisho miaka 5 ya ITM Tanzania Limited, kampuni ya huduma ya rasilimali watu. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki na DAS wa Ilala akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila.

Selemani alisema, “soko la ajira au tuseme, sekta hii ni moja ya sekta muhimu sana katika uchumi wetu, kunapokuwa na ukuaji wa sekta hii, tunaona ukuaji wa uchumi pamoja na ukuaji wa pato la kila mtu.

Mwenyekiti wa kampuni mama ya ITM Tanzania, Sylva Monga akizungumza na wageni waalikwa kwenye hafla hiyo.

Hivyo ni muhimu kabisa kwa serikali kuendelea kufanya kazi kwa karibu na wadau kama vile ITM Tanzania ambao wanaweza kuchangia ukuaji katika kukuza vipaji vyetu vya ndani na kuwasaidia kushindana katika ngazi ya kimataifa.”

Waliohudhuria ni Mwenyekiti wa ITM Holdings, Sylva Monga, wafanyakazi wa ITM Tanzania Limited, wawakilishi kutoka kampuni za ITM kutoka nchi nyingine ambako ITM ina uwakilishi.

Kwa upande wake, Meneja wa ITM Tanzania, Adelaida Kwayu aliishukuru serikali kwa kuendelea kusaidia katika ukuaji wa sekta hiyo na kusema; “Ninajivunia kueleza kuwa ITM Tanzania imefanikisha kuajiri zaidi ya watu 1,000, na kuwaunganisha watu wenye vipaji na mashirika yanayotambua uwezo wao.

Wafanyakazi wa ITM Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mgeni rasmi, Katibu Tawala wilaya ya Ilala, Charangwa Selemani (mwenye koti nyekundu) kwenye hafla hiyo.

Kwa kuongezea, kwa sasa tuna zaidi ya wafanyakazi 500 waliopewa kazi na mashirika ya nje, wakiyapa mashirika kubadilika na usaidizi wanaohitaji ili kustawi”. Alimaliza kusema.

ITM Tanzania ni kampuni tanzu ya ITM Holdings, yenye makao yake makuu nchini DRC Congo. Kundi hilo la makampuni lina nyayo katika nchi mbalimbali zikiwemo DRC, Rwanda, Tanzania, Nigeria, Benin, Togo, Senegal, Uganda, Kenya, Angola, na Ujerumani.

Leave A Reply