Ivo Mapunda: Manula wa Azam Sio wa Simba

 

KIPA wa zamani wa Yanga, Ivo Mapunda akiwa na kipa wa Simba, Aishi Manula (kulia).

KIPA wa zamani wa Yanga, Ivo Mapunda amesema kuwa kiwango kinachoonyeshwa na kipa wa Simba, Aishi Manula kwa sasa ni tofauti na alivyokuwa Azam FC, hivyo anahitaji kujiimarisha zaidi.

 

Manula alitua Simba mwanzoni mwa msimu huu akitokea Azam FC ambapo anategemewa katika kikosi cha timu ya taifa.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Mapunda amesema kuwa, kiwango kinachoonyeshwa na Manula kwa sasa si kile alichokuwa akikionyesha alipokuwa Azam na kudai kuwa anahitaji kufanya mazoezi na kujituma ili aweze kuwa bora kama ilivyokuwa awali ijapokuwa hajashuka sana.“Kiwango kinachoonyeshwa na Manula kwa sasa ni tofauti na alivyokuwa Azam japokuwa sio kizuri sana wala kibaya sana, lakini kwa sasa kimeshuka.

 

“Inawezekana ni mfumo uliokuwepo katika timu yake, lakini mwalimu aliyekuwa naye ni mzuri wakati mwingine anapotea wakati mwingine anarudi kuwa sawa.

 

“Ni kipa ambaye huwa namuamini sana kwani kufanya makosa kwake huwa ni nadra sana, nikizungumzia kwa upande wa makipa wengine nawaona wote wanafanya vizuri japokuwa sijaona yule mwenye kiwango kilekile muda wote.

 

“ Makipa wote hawapishani viwango na siku zote ili uweze kuwa vizuri ni lazima ujitume ukubali kuumia. Ukitaka kufanya vizuri lazima ufanye mazoezi sana,” alisema Mapunda.

HABARI NA KHADIJA MNGWAI | SPOTI XTRA


Loading...

Toa comment