The House of Favourite Newspapers

Iyanya: tiketi ya Kcee ndiyo ilinifikisha Lagos kwa mara ya kwanza

0

iyyIyanya akiwa na Kcee.

Lagos Nigeria

SI watu wengi wanafahamu kwamba safari ya kwanza ya Iyanya Onoyom Mbuk, kiongozi wa kundi la Made Men Music Group (Triple MG) kwenda jijini Lagos iligharimiwa na Kingsley Chinweike Okonkwo, ambaye anafahamika zaidi kama KCee. Mwimbaji huyo maarufu kwa kibao cha ‘Limpopo’, ndiye aliyemleta Iyanya jijini Lagos kutoka Calabar, Jimbo la Cross River.

Kcee-Iyanya-HarrySongIyanya alifichua hilo wakati wa kuzindua albamu yake ya nne iitwayo ‘Applaudise’ katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa klabu ya ThisDay Dome jijini Abuja, siku ya Jumamosi.

Mwanamuziki huyo maarufu kwa kibao chake cha ‘Kukere’, alimtambulisha KCee jukwaani ili kumshukuru kwa kitendo hicho alichokionyesha miaka kadhaa iliyopita.

Iyanya aliwahi kufanya kazi katika baa moja huko Calabar miaka mingi iliyopita kabla hajajikita katika muziki.

Leave A Reply