IYOBO, AUNT ‘FULL’ KURUSHANA ROHO

DANSA wa Kundi la Wasafi Classic Baby ‘WCB’, Moses Iyobo ‘Moze’ na mzazi mwenziye Aunt Ezekiel ambao sasa wamemwagana, hivi karibuni walionekana kurushana roho baada ya kukutana kwenye bethidei ya Tanasha Donna na mama Nasibu Abdul ‘Diamond’, Sanura Kassim ‘Bi Sandra’.

 

Tukio lilichukua nafasi katika Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar ambapo Moze ndiye aliyeanza kuwasili kwenye ukumbi huo akiwa na mrembo wake aliyedamshi ile mbaya hali iliyosababisha wapiga chabo wagune na kusema; “mmmh hapa sasa kazi ipo.”

 

Wawili hao waliingia ukumbini hapo kwa kushikana mikono na kwenda kukaa katika eneo lao. Iyobo na Aunt ni kama walikuwa wakiviziana mara paaap, Aunt naye huyo na mkaka mtanashati wakaingia ukumbini hapo wao kwa mbwembwe zaidi wakiwa wanatembea huku kama wanalaliana.

Mambo ya kurushana roho Moze na Aunt hayakuishia hapo, wakiwa ukumbini, kila mmoja alikuwa akibadilisha mikao na mtu wake huku mambo ya kufutana jasho yakichukua nafasi kila wakati licha ya kuwepo kwa kipupwe kikali ukumbini humo.

 

Licha ya wawili hao kutotaka kuzungumzia lolote, ilielezwa kuwa Aunt na jamaa huyo hawakuwa na uhusiano wa kimapenzi bali ilikuwa ni kampani tu vivyo hivyo kwa Iyobo.
Toa comment