The House of Favourite Newspapers

IZZO B AMFUNGUKIA SEPENGA

Izzo Business ‘Izzo B’.

MWANZONI mwa miaka ya 2,000 kulizuka makundi na wasanii ambao walikuwa wakiiwakilisha mikoa yao katika muziki wa Bongo Fleva.

Ukienda Tanga lazima utamzungumzia Matonya, Bwana Misosi, MwanaFA, Cassim Mganga na Wagosi wa Kaya, lakini ukimba Arusha, utazungumzia Nako 2 Nako Soldiers na Weusi na ukienda Morogoro lazima utamzungumzia Afande na Belle 9, Dodoma Chamber Squad, Makole Hexagon, ukienda Mtwara kuna Z-Anto wakati Mwanza kuna Fid Q, Kala Jeremiah na wengine wengi.

 

Ndani ya Jiji la Mbeya napo kulikuwa na vichwa ambavyo ni Quick Rocka, Sugu pamoja na Izzo Business ‘Izzo B’. Kwa muda mrefu Izzo B amekuwa akiliwakilisha jiji lake hilo ambapo kila mwisho wa mwaka huenda kufanya shoo kubwa maalum kushea na mashabiki wake huko. Kupitia kupenda alipotokea, amefanikiwa kutengeneza tisheti kwa ajili ya kulitangaza jiji hilo ambapo tisheti hizo anaziita Home Sweet Home na Mbeya City.

 

Baada ya kubamba na ngoma kibao ikiwemo Kidawa, Tumoghele na Rimoti, kwa sasa Izzo B anakimbiza kwenye muziki akiwa na Ngoma ya Nishadata.

Showbiz imefanya naye mahojiano exclusive kuhusu maisha yake ndani na nje ya muziki, huyu hapa;

Showbiz: Tungependa kujua uhusiano wako na Bella Music uliyekuwa ukiunda naye kundi moja la The Amazing maana hujawahi kuzungumzia chochote hata baada ya kujifungua…

 

Izzo B: Na bado sitaweza kuzungumza chochote kwa sasa kwa sababu kuna vitu ambavyo inabidi vifuatwe kisheria pande zote za familia, vikishakaa sawa, basi nitazungumza.

Showbiz: Suala la ndoa?

Izzo B: Bado kuna vitu vinajadiliwa na familia kwa hiyo siwezi kuongeza kitu.

Showbiz: Vipi kuhusu watoto maana walikuwa wanasema siyo wa kwako?

Izzo B: Watoto ni wangu, hilo mbona halina ubishi…

 

Showbiz: Kwa nini usipotoa wimbo unapotea husikiki kabisa hadi utoe wimbo mwingine?

Izzo B: Unajua kila mtu ana life style yake ambayo yeye anapenda kuishi na mara nyingi huwa mimi sipendi kuishi uongo, mimi napenda kuishi maisha yangu ambayo nayamudu siyo ya kujioneshaonesha kama sina kitu cha umuhimu au ulazima wa kufanya hivyo.

Showbiz: Mbali na muziki ni kitu gani kingine unafanya?

 

Izzo B: Nina biashara zangu ndogondogo tu ambazo zinanikidhi mahitaji ninayoyahitaji na maisha yanaendelea.

Showbiz: Siku hizi haupo karibu na rafiki yako, Quick Rocka, vipi kuna tatizo lolote kati yenu?

IzzoB: Hapana labda kama watu hawajatufuatilia tu, sisi bado ni marafiki sana, tena tunatoka sehemu moja, sisi ni kama ndugu, yaani hatuwezi kuwa na bifu na hata hapa nimetoka studio kwake labda hawajatuona muda mrefu kwenye TV ila wasijali kuna projekti yangu na yeye inakuja wakae tayari.

Showbiz: Kwa nini haupo karibu na wasanii wenzako kama umejitenga f’lani hivi?

Izzo B: Hapana, mbona mimi nipo na ninajichanganya sana na washikaji wala sina tatizo sasa kwa nini nijitenge na watu ambao tunafanya kazi ya aina moja maana mnapokutana mnabadilishana mawazo na lazima utatoka na kitu ulichojifunza. Kwa ufupi sijitengi nipo sana ila ‘lowkey’ siyo mpaka watu wajue.

 

Showbiz: Unaamini katika kiki kama ambavyo wasanii wengi siku hizi hufanya?

Izzo B: Siamini sana kwenye kiki kwa sababu siku zote kazi nzuri inajiuza tu hata bila kiki. Unajua kiki ni ‘fifty fifty’ inaweza ikakupandisha unapotaka au ikakushusha tofauti na pale ambapo ulikuwepo na kila mtu ana mazingira na staili ambayo alianza sanaa yake kwa hiyo mimi kiki hapana kwakweli, kazi kama nzuri watu watasapoti tu ikiwa haijafikia kiwango, basi tutarudi studio kufanya kazi mpya.

Showbiz: Una kipi cha kuwashauri wasanii wanaopenda kiki?

 

Izzo B: Mimi ninawashauri wasiendekeze sana kwenye kiki kwa sababu kuna muda hata unaweza usipate shoo kwa sababu ya hizo kiki au wanaweza wakakosa madili ya makampuni makubwa kwa sababu ya kiki zisizo na maana. Ni kampuni gani itataka kuonekana ya kijinga kwa kuwaita watu wenye kiki za kipumbavu, halafu watu washashtuka kwa sababu imekuwa too much hadi wameshazoea na kuona kawaida, kikubwa ninawashauri wasanii wenzangu tufanye muziki mzuri tu.

 

Showbiz: Izzo ni mtu wa aina gani?

Izzo B: Ni mtu poa sana, hanaga shida na mtu, anapenda kujichanganya na watu, anapenda sana familia yake.

Showbiz: Ukipata nafasi ya kumshauri kitu chochote Wema Sepetu ‘Sepenga’ kwa ishu ambayo anaipitia sasa hivi utamshauri nini?

 

IzzoB: Naweza nikasema awe makini sana kutokana na pozisheni ambayo anayo kwa sababu yeye ni brand, anafahamika sana, kuna watu wengi ambao yeye ‘anawa-inspire’ na wengi wanamtazama yeye na kama unavyojua siku hizi kwenye mitandao hadi watoto wa chini ya miaka kumi na nane wapo na wanam-follow Wema kwa sababu wanatamani kuwa kama yeye. Kwa hiyo ushauri wangu ni vitu binafsi kama vile vibaki kuwa binafsi tu, kujirekodi hukatazwi, weka katika sehemu ya siri ili uangalie wewe, lakini siyo mpaka kuvitoa nje siyo kitu kizuri.

SHAMUMA AWADHI

Comments are closed.