The House of Favourite Newspapers

Izzo Bizness Akiri Skendo Kumrudisha Nyuma

BONIPHACE NGUMIJE | RISASI JUMAMOSI | Mikito Nusunusu| DAR ES SALAAM

MKALI wa michano Bongo, Emmanuel Semwinga ‘Izzo Bizness’ amefunguka kuwa ameamua kuachana na skendo kwa sababu zinamrudisha nyuma.

Akibonga na Mikito Nusunusu, Izzo Bizness alisema masuala ya skendo au kuzungumzia wimbo ambao bado ndiyo yupo kwenye maandalizi yamekuwa yakimrudisha nyuma kwani wakati mwingine katika hali iliyo nje ya uwezo wake anajikuta akikwama kuuachia kama alivyowaahidi mashabiki jambo ambalo linawachanganya mno.

“Mambo ya skendo au kuzungumzia kazi ambayo bado haijakamilika nimeamua kuyakacha kabisa, yanapunguza mashabiki maana wakati mwingine tunakuwa tunawachanganya na wanatuona waongo hasa pale tunaposhindwa kutimiza ahadi kwa wakati,” alimaliza Bizness.

Comments are closed.