The House of Favourite Newspapers

Izzo business: Ubabaishaji kwenye tasnia ya muziki unakera

0

IzzooooMSANII wa Hip Hop nchini Emmanuel Semwinga ‘Izzo Business’ hivi karibuni ametoa dukuduku lake la moyoni kwa kusema kuwa anachukizwa na mfumo wa uendeshwaji wa tasnia nzima ya muziki nchini ambao unashindwa kuwapiga tafu zaidi wasanii ili waweze kupiga hatua kubwa kiasi cha kuyafikia mafanikio ambayo wanatakiwa kuyapata kupitia kazi zao.

Akizungumza hayo na mwandishi wetu, Izzo ambaye alitamba na Wimbo wa Rizi One alisema kwamba ubabaishaji wa waendeshaji ndiyo unaowafanya kuwa kwenye hali hii hivyo anaomba Mungu achaguliwe kiongozi mwingine ambaye ataendeleza pale alipoishia Jakaya Kikwete ili wapate maisha bora zaidi.

“Kwenye tasnia ya muziki kuna ubabaishaji mkubwa unaendelea, mara kwa mara nimekuwa nikijiuliza kwa nini mfumo wa kuuza album ulipigwa chini lakini sipati sababu za msingi, unajua shoo ni vigumu sana kuwapa manufaa wasanii wote kutokana na uhaba wa waandaaji wa matamasha kwa hiyo kuna kila sababu ya wadau wa muziki Tanzania kuliangalia hilo.”

Leave A Reply