The House of Favourite Newspapers

Jack Chuz alia na wasambazaji

0

 

JACKYWACHUZII.jpgNYOTA wa filamu, Jacqueline Pentzel maarufu kama Jack Chuz amesema wasambazaji wa kazi za wasanii ndiyo wanaoharibu soko lao, kiasi kwamba hivi sasa sanaa hiyo ni kama inapumulia mashine.

Akizungumza na gazeti hili, Jack Chuz alisema soko lao limeshuka sana lakini wasambazaji hao ambao wamekuwa wakiwanyonya hawana msaada wowote kwao, hivyo kuufanya mwelekeo wao kuwa mbaya.

“Ninaiomba serikali iangalie na huku kwetu wasanii, maana tunapoelekea ni pabaya, tumechoka kuwatumikia watu wasio na huruma, hawa wasambazaji ndiyo chanzo kikuu cha tasnia ya filamu kushuka kwani wananufaika wao zaidi wakati sisi tunaumia,” alisema Jack Chuz.

JIUNGE NA GLOBAL BRAKING NEWS

GLOBALBREAKINGNEWS100.jpg

Leave A Reply