The House of Favourite Newspapers

Jack Dustan: wanaojichora ‘tatuu’ za wapenzi wanajichafua

0

IMG_0016

Mrembo aliyejipatia umaarufu kupitia Shindano la Maisha Plus, Jacqueline Dustan ‘Jack’

Stori: Imelda Mtema

SOMO! Mrembo aliyejipatia umaarufu kupitia Shindano la Maisha Plus, Jacqueline Dustan ‘Jack’ ameweka wazi kuwa baadhi ya mastaa wanaojichora ‘tatuu’ za majina ya wapenzi wao ni kujichafua kwa sababu wanapoachana wanapata tabu kuzifuta.

kizungumza na gazeti hili, Jack alisema kwamba, katika maisha yake hawezi kujichora jina la mwanaume kwa kuwa siku hizi mapenzi hayana muamana na wakati wowote kuna kuachana huku ukijikuta mwili mzima umejichora jina la mpenzi wako.

Baadhi ya mastaa waliojichora majina ya wapenzi wao ni pamoja Nuh Mziwanda aliyejichora jina la Shilole na Quick Rocka aliyejichora jina la Kajala Masanja.

Leave A Reply