Jack Ma Awashauri Wafanyakazi Kufanya Mapenzi Mara 6 kwa Wiki

 

Tajiri wa China na mmiliki wa kampuni ya Alibaba Group Jack Ma amewasisitiza wafanyakazi wa maofisini kufanya mapenzi angalau mara 6 kwa wiki akidai itawaongezea ufanisi mzuri wa kazi za ofisi na maisha ya kawaida.

 

Jack Ma mwenye utajiri wa Tsh. Trilioni 88, awali aliwahimiza watu kufuata falsafa aliyoiita ni “996” (kufanya kazi 9:00 hadi 9:00, siku 6 kwa wiki mahali pa kazi yaani (kuaznia saa 3:00 asubuhi hadi saa 3:00 usiku), wakati akifanya mkutano wa wafanyakazi wa kampuni yake aliitambulisha falsafa ya “669” ambapo ni kufanya mapenzi mara 6 ndani ya siku 6 kwenye mfumo wa masaa 12 ya kazi kwa China.

 

Ma mwenye umri wa miaka 54 alikuwa akizungumza katika kikao cha kampuni yake ambayo hufanyika kila mwaka kwenye “Siku ya Ali” Mei 10 katika makao makuu ya kampuni huko Hangzhou.

Loading...

Toa comment