Jada Pinkett Azungumzia Alivyokwepa Mawazo ya Kujiua

Jada Pinkett Smith.

MSANII wa Marekani, Jada Pinkett Smith ambaye ni mwimbaji, mnenguaji, mwigizaji na mjasiriamali, amezunguzia jinsi alivyokwepa,  hapo nyuma, mawazo mabaya yaliyomfanya atake kujiuua.

Mwaamke huyo ambaye ni mke wa msanii mwingine maarufu wa Marekani, Will Smith, ameyasema hayo kufuatia kujiua siku za karibuni kwa Kate Spade (mwanamitindo na mfanyabiashara) na Anthony Bourdain (mtunzi, msanii, mwigizaji na mjasiriamali), wote wa Marekani.

Jada majuzi aliandika katika mtandao wake wa Instagram kwamba:

“Kujiua kwa Kate na Anthony, kumenikumbusha nilivyokuwa nimekata tamaa na kufikiria kila mara kujiua pia…  Katika miaka niliyokwepa jambo hilo, miezi mingi iliyopita,  nilitambua akili na moyo vinaweza kuwa dhaifu bila msingi wa roho yenye nguvu.  Ninachokula, ninachotazama kwenye televisheni, muziki ninaosikiliza, ninavyojali mwili wangu, vitendo vyangu vya kiroho,  watu nilio karibu nao, mfadhaiko wa mwazo nilio nao na kadhalika… vyote kudhoofisha afya yangu ya akili.  Afya ya akilini ni wajibu wangu kila siku.  Ni wajibu wenye upendo mkubwa.  Kate na Anthony wapumzike kwa amani.  Wengi wanaweza wasifahamu…lakini nafahamu, na asubuhi hii nina furaha kubwa niliweza kushinda.”

“With the suicides of Kate and Anthony, it brought up feelings of when I was in such despair and had considered the same demise…often. In the years I spent towards my healing, many moons ago, I realized the mind and heart can be extremely delicate without the foundation of a formidable spirit. What I eat, what I watch on TV, what music I listen to, how I care for my body, my spiritual practice, what people I surround myself with, the amount of stress I allow and so on… either contribute to or deteriorate my mental health. Mental health is a daily practice for me. It’s a practice of deep self-love. May Kate and Anthony Rest In Peace. Many may not understand… but I do, and this morning I have the deepest gratitude that I pulled through.”

 

Loading...

Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment