JAFFERJEE: MABINGWA WA VIFAA VYA USALAMA MAHALI PA KAZI

Hakuna shughuli ngumu kama uendeshaji wa mitambo mikubwa, kufanya kazi viwandani, migodini au kwenye miradi mikubwa ya ujenzi wa maghorofa, nyumba za kawaida na miundombinu kama madaraja na kadhalika.

 

Usalama kazini huwa ni changamoto kubwa kwa watu wanaofanya kazi kwenye sekta hizi na upo ushahidi wa watu wengi ambao wamepoteza maisha au kupata ulemavu wa kudumu, kwa sababu ya ajali zinazotokea mahali pa kazi.

Changamoto hizi ndiyo zilizoifanya kampuni ya Jafferjee Hardware and Machinery (JHM), kuamua kuwekeza nguvu zake zote kuwasaidia Watanzania kwa kuhakikisha kwamba ajali au madhara wanayoyapata wafanyakazi wa sekta za viwandani na ujenzi, zinapungua sana na hata zinapotokea, basi madhara yake yanakuwa madogo.

 

Kivipi? Jafferjee Hardware and Machinery, wanauza na kusambaza vifaa mbalimbali vya usalama maeneo ya kazi nchi nzima, kwa bei nafuu ambayo kila mtu anaweza kumudu wakiwemo waajiri, kwa ajili ya usalama wa wafanyakazi wawapo maeneo ya kazi.

“Tunawahudumia wafanyakazi wa sekta zote, kuanzia mtu mmojammoja, kampuni ndogo, za kati na kubwa, taasisi za serikali na binafsi kwenye nyanja za ujenzi, viwandani, migodini, kwenye mafuta na gesi, usafirishaji, kwenye sekta za kilimo, afya, ulinzi na usalama na kadhalika,” amesema Shabbir Jafferjee, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya JHM na kuongeza:

 

“Vifaa vinavyopatikana kwetu ni pamoja na kofia ngumu (helmets), vifaa vya kulinda macho na masikio maeneo ya kazi za hatari kama welding glasses, welding shield, miwani ya kuyakinga macho na mionzi mikali ya moto, kofia zenye tochi kwa wafanyakazi wa migodini na viwandani, mask za kuzuia hewa za sumu na vumbi, mitungi ya hewa ya oksijeni na gloves za aina zote.

“Pia tunavyo vifaa kama maovaroli maalum yenye uwezo wa kuukinga mwili na madhara, reflective vests, makoti ya mvua, sare za askari wa makampuni ya ulinzi, reflective belts na mablanketi maalum yenye uwezo wa kumkinga mtu dhidi ya moto, gum boots, vifaa vya kubaini uvujaji wa gesi na mionzi hatari, dustbins, fire extinguishers na vifaa vingine vingi, vya kila aina na tunamfikishia mteja wetu mahali popote alipo hapa nchini.”

 

Jafferjee Hardware and Machinery wanafanya kazi kwa kushirikiana na kampuni kubwa duniani, ACME ya nchini India na MIDAS ya Canada, ambayo ina matawi yake kwenye nchi za India, Pakistan, China, Bangladesh, Taiwan na Malaysia. Kampuni hizi mbili, zimejijengea heshima kubwa duniani kote kwa utengenezaji na uuzaji wa vifaa vya usalama mahali pa kazi.

Kwa jijini Dar es Salaam, Jafferjee Hardware and Machinery wanapatikana Block 32, Plot 53, Mtaa wa Kipata, Kariakoo na plot 1720, Barabara ya Haille Selassie, Masaki jijini Dar es Salaam, wanatazamana na Marrybrown au unaweza kuwasiliana nao kwa namba za simu 0753600099, 0714826020 au 0787522672.

 

Pia unaweza kuwasiliana nao kwa anuani ya barua pepe, info@jhmsafety.co.tz, sales@jhmsafety.co.tz na marketing@jhmsafety.co.tz. Unaweza pia kutembelea mtandao wao kupitia anuani ya www.jhmsafety.co.tz ili kujionea mwenyewe bidhaa bora na huduma wanazozitoa.

Na Mwandishi Wetu


Loading...

Toa comment