The House of Favourite Newspapers

Jafo Ataka Soko la Mabibo Lijenge Miundombinu Bora

…Akitembelea soko hilo.
Waziri Suleiman Jafo akisaini kitabu cha wageni katika soko la ndizi la Mabibo jijini Dar es Salaam leo. 
…Akizungumza na wafanyabiashara na wananchi wa soko hilo.

 

Akijionea hali halisi ya mazingira ya soko la Mabibo.

 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Suleiman Jafo, ametembelea soko la ndizi la Mabibo jijini Dar es Salaam ambapo ameitaka Halmashauri ya Wilaya ya Ubungo kujenga miundombinu rafiki ya maji-taka katika soko hilo ili kuliweka katika mazingira salama.

 

Jafo amesema hakufurahishwa na  miundo mbinu ya soko hilo kwani kumejaa tope na uchafu na kusababisha mifereji kuziba. Waziri huyo pia alisema kwamba mapato ya Sh. milioni 90 yanayokusanywa kwa mwezi hayaridhishi, hivyo aliwataka wabuni mipango ya kuweza kuyaongeza mapato hayo.

 

NA DENIS MTIMA/GPL

 

Comments are closed.