Jaguar Akamatwa Bungeni, Serikali ya Kenya Yamkana – Video

MBUNGE  wa Jimbo la Starehe, Nairobi Kenya, Charles Njagua ‘Jaguar’,  amekamatwa leo Juni 26, 2019 kwa amri ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) wa nchi hiyo baada ya kutoa kauli ya kibaguzi dhidi ya Watanzania, Wachina na Waganda waishio Kenya.

 

Jaguar amekamatwa nje ya ukumbi wa Bunge na kupelekwa kituo cha polisi ambacho bado hakijatajwa.

 

Serikali ya Kenya imewahakikishia ulinzi wageni wote wanaoingia na kuendesha shughuli za kibiashara nchini humo baada ya maneno ya vitisho aliyoyatoa Jaguar.

 

Msemaji wa serikali nchini Kenya, Cyrus Oguna, amethibitisha kuwa kauli ya Jaguar si msimamo wa serikali ya Kenya na hivyo amepinga vikali msimamo wa mbunge huo.

Aidha, Oguna ameongeza kwa kusema Wakenya ni watu wasio na ubaguzi na taifa lolote lile hivyo wageni kutoka nchi mbalimbali wasiwe na hofu kuhusu ulinzi wao.

 

Jaguar alikaririwa akizungumza maneno yenye vitisho kwa wageni kupitia kipande cha video kilichosambaa siku ya Jumatatu.


Loading...

Toa comment