The House of Favourite Newspapers

Jahazi Kulisimamisha Jiji

0

NA MWANDISHI WETU | SHOW BIZ

Bendi ya Jahazi Modern Taarab ikiongozwa na mastaa wake, Leila Rashid, Amigo, Mwasiti Kitolonto, Ally J, Fatuma Kassim na wengine kibao imepania kulisimamisha Jiji la Dar katika onesho kabambe litakalofanyika Jumamosi ya mwisho wa mwezi huu, Aprili 29 katika Uwanja wa Burudani wa Taifa wa Dar Live uliopo Mbagala- Zakhem, Dar.

Akizungumza na Showbiz Xtra, kiongozi wa bendi hiyo, Amigo alisema katika onesho hilo wamejipanga kufanya vitu tofauti ili kuunogesha usiku huo na kuwataka mashabiki wa Taarab kujitokeza kwa wingi.

“Tutalisimamisha Jiji la Dar kwa muda kwa kufanya mambo tofauti kabisa na waliyoyazoea, mashabiki wetu wote waje kwa wingi,” alisema Amigo.

Naye Meneja wa Dar Live, Juma Mbizo alisema kuwa kiingilio cha onesho hilo ni shilingi 6,000 tu lakini burudani itakuwa bab’ kubwa.

“Siku hiyo Jahazi watatoa burudani nzuri na yenye kufurahisha kwa shilingi 6,000.

Wakati huohuo:

Madee

MADEE, DOGO DITTO JUKWAA MOJA DAR LIVE

RAPA Madee, Young Killer, Country Boy na Chemical Aprili 30, mwaka huu (Jumapili hii) watadondosha bonge la shoo kwenye jukwaa la Dar Live.

Wasanii hao watafanya shoo iliyopewa jina la Walimende Concert iliyoandaliwa na Kituo cha Radio cha EFM kwa kupitia kipindi cha Ladha3600.

Dogo Ditto.

Akizungumza na Showbiz Xtra, Mratibu wa Shoo hiyo, Jabir Saleh a.k.a Kibonge Tozi alisema siku hiyo ya shoo Kipindi cha Ladha3600 kinatimiza mwaka mmoja, hivyo kwa kushirikiana na Dar Live wamepanga kutoa burudani ya nguvu.

“Tunajivunia kutimiza mwaka mmoja, tunarudisha fadhila kwa wasikilizaji wetu, wasanii wengine watakaoipamba shoo hiyo ni Dogo Ditto, Pam D, Chin Beez, Tammy the Baddest na Hussein Machozi atakayefanya shoo yake ya kwanza nchini akitokea Italia.

“Burudani nzima itadodoshwa na madjs kutoka EFM nikiwemo mimi mwenyewe (Kibonge Tozi) , Rdj Blackiie, Rdj Spar na Samio Love watakaoporomosha shoo hiyo,” alisema Kibonge Tozi

Leave A Reply