The House of Favourite Newspapers

Jahazi kurudi kwa kishindo Dar Live

0

jahazi+PICKUNDI la Muziki wa Taarab lisilo na mpinzani Bongo, Jahazi Modern Taarab likiongozwa na Mfalme Mzee Yusuf, Agosti 20, mwaka huu linatarajiwa kurudi kwa kishindo ndani ya Uwanja wa Kimataifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar kutoa bonge moja la shoo.

Meneja wa Dar Live, Juma Mbizo aliiambia Showbiz kuwa usiku huo Jahazi watakamua nyimbo zao zote kali mpya na za zamani zinazobamba wakiwa na wakali kama Leyla Rashid, Fatma Shobo, Rahma Machupa, Fatma Kassim na wengine kibao.

“Utakuwa usiku wa toa kitu weka kitu, Jahazi kama wanavyojulikana siyo watu wa kubahatisha. Usiku huo zitapigwa kuanzia Mahaba Niue, Nina Moyo Siyo Jiwe, Nia Safi Hairogwi, Kamwe Sitaumbuka, Kaning’ang’ania Mpenzi Chocolate na nyingine nyingi,” alisema Mbizo.

Pia kwa mara ya nyingine wakali wapya, Aisha Vuvuzela na Zubeda Mlamali watalivamia jukwaa.

Leave A Reply