The House of Favourite Newspapers

Jahazi Lazidi Kuandamwa na Jinamizi

Othman Soud ‘Amigo’ au ‘Prince’.

 

KUNDI la Jahazi Modern Taarab limezidi kupata jinamizi la kukimbiwa na wanamuziki wake tangu kiongozi na mwanzilishi wake, Mzee Yusuf ‘Mfalme’ alipoamua kumrudia muumba wake ambapo hivi karibuni mrithi wa nyimbo zake aliyemuacha kundini hapo, Othman Soud ‘Amigo’ au ‘Prince’ naye aliondoka.

 

Baada ya Mzee kuondoka, Amigo aliliziba pengo lake ambapo alikuwa akiimba vibao vyote vikali vya Mzee, lakini naye ameamua kujiondoa kwenye kundi hilo.

Amigo alilithibithishia Ijumaa Wikienda kuwa, ameondoka kwenye kundi hilo huku akiitaja sababu kubwa kuwa ni kutafuta maslahi zaidi kwani yuko mbioni kuanzisha kundi lake.

 

“Ni kweli nimeachana na Jahazi. Niko kwenye mikakati ya kuanzisha kundi langu,” alisema Amigo.

Wanamuziki wengine waliolihama kundi hilo baada ya kuondoka Mzee ni Mwasity Robert, Miriam Amour, Leyla Rashid na wengineo.

Richard Bukos

 STORI: Imelda Mtema, Dar, IJUMAA WIKIENDA

LIVE: Sherehe ya Ndoa ya Shilole Usiku Huu Masaki Part – 2

Comments are closed.