The House of Favourite Newspapers

Jaji  Bomani Alaani  Mauaji na Ukatili kwa Wakulima na Wafugaji

0

 

1.Jaji Bomani akisoma taarifa yake kwa wanahabari (hawapo pichani).Jaji Bomani akisoma taarifa yake kwa wanahabari (hawapo pichani).2.Mwanasheria mstaafu wa  serikali, Jaji Mack Bomani akitoa ufafanuzi wa jambo kwa wanahabari (pichani hawapo).…Akitoa ufafanuzi wa jambo.3.Wanahabari wakichukua tukio hilo.Wanahabari wakichukua matukio katika hafla hiyo.

MWANASHERIA  Mkuu  Mstafu wa Serikali, Jaji Mark Bomani amelaani vitendo vya mauaji dhidi ya watu  na mifugo.

Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam, Jaji Bomani amesema kuwa hivi karibuni kumejitokeza wimbi la vikundi vya watu vinavyofanya vitendo vya ukatili hususani upande wa wafugaji na wakulima kugombania mashamba na hatimaye kuuana na kuua  mifugo.

Bomani amesema zaidi ya ng’ombe  70 hivi majuzi waliuawa na watu  kadhaa wakajeruhiwa huko Mvomero, Morogoro, kutokana na migogoro ya wakulima na wafugaji, jambo ambalo linabidi  kudhibitiwa lisiendelee kujitokeza kwenye jamii.

Aidha amesema miongoni mwa makundi hayo yamekuwa yakiharibu mimea kwa kuikata na kuichoma  zikiwemo nyumba za wawekezaji ambapo ameitaka serikali kuchukua hatua kali dhidi ya vitendo hivyo.

Vilevile amesema serikali inapaswa kuweka vipaumbele vya hali ya juu katika kuhakikisha inatatua migogoro iliyopo baina ya wafugaji na wakulima kwenye jamii husika ili kupunguza vitendo vya kikatili vinavyoendelea kushamiri.

Na Denis Mtima/GPL

Leave A Reply