The House of Favourite Newspapers

Jaji Msuya kuzikwa Jumamosi, Dar

0

Mwili wa aliyekuwa Jaji wa mahakama kuu ambaye amejiuzulu  hivi karibuni, Upendo Msuya unatarajiwa kuzikwa Jumamosi katika makaburi ya Kinondoni saa 9 mchana.

Jaji Msuya alifariki Jana   katika hospitali ya Kairuki alipokuwa amelazwa akiugua ugonjwa wa Kiharusi.

Msemaji wa familia ambaye pia ni mume wa marehemu Mhandisi Hilary Msuya  amesema misa ya kumuaga marehemu itafanyika Kanisa la KKKT Wazo Jumamosi asubuhi

“Jumamosi asubuhi tutafanya ibada fupi hapa nyumbani na baadaye tutaelekea kanisani kwa ajili ya misa”amesema.

 

LIVE: Rais Magufuli, Pierre Nkurunzinza Wawahutubia Wananchi Ngara – Kagera

Leave A Reply