The House of Favourite Newspapers

Jamani Antiii…Nishushe Ununio..!-16 …Mwisho

ILIPOISHIA RISASI MCHANGANYIKO:

“Vivian wewe ni kati ya wasichana warembo wenye kumvutia kila mwamaume! Umeumbwa ukaumbika mamaa! Nakuomba kwa muda huu tukumbushie yale mambo yetu ya zamani kipindi kile tumeanza uhusiano,” Rama kwa mara ya kwanza alishindwa kuzuia hisia zake na kujikuta akishikilia mapaja ya Vivian…

Vivian akajitahidi kupingana naye lakini akashindwa kwa sababu kile kinywaji kilimtuma Rama kuhama eneo la mapaja na kuelekea katika kifua cha Vivian hali iliyomfanya kuwa mpole na kumuacha kutazama idara nyeti…

MALIZANA NAYO SASA…

VIVIAN hakuwa na namna tena. Akamuacha Rama aendelee na alichokuwa anakifanya, ingawa kuna mahali alilazimika kumzuia kwa nguvu kutokana na kuzidiwa na ujuzi wa Rama, yote haya aliyafanya lakini kwa geresha tu, moyoni alianza kusikia kiu ya kukunwa kwa nazi yake.

Rama hakuwa na aibu wala simile. Tayari ubongo wake ulishachanganyikana na maji yenye kimea na kuondoa kabisa uwezo wa kujidhibiti ukizingatia ukweli kwamba hakukuwa na chochote kigeni mwilini mwa Vivian kwani walishakuwa wapenzi kipindi ambacho wote walikuwa wageni wa Jiji la Dar, ndiyo kwanza walikuwa na Krismasi moja wakiwa mjini.

“Rama bwana, nini lakini…. Mimi sitaki ujue,” Vivian alianza kulalama kimahaba huku akijikunjakunja kufuatia vidole vya Rama kuanza kugusa maeneo yenye shoti za umeme na ziletazo hatari zaidi mwilini mwake, mwenye asili ya Tanga, mkoa ambao unasadikiwa umejaaliwa wakazi wenye ujuzi wa mahaba na mapenzi. Ninaposema mahaba na mapenzi msomaji, lazima ujue kwamba nazungumzia mambo makubwa mawili totauti.

Mahaba ni yale manjonjo ya wapenzi waonyesheapo wakiwa wawili kwenye eneo husika na mapenzi ni zile hisia za ndani wa moyo wa mtu kwa mwingine.

Rama alizidisha utundu na kuanza kumkabili mwanamke wa watu kwa hali ya kujiamini zaidi. Ikafika mahali wote wawili wakaweka aibu pembeni, vigezo na masharti pembeni, Viviana akajiachia kwelikweli na Rama akaamua kumkabili kiume kwelikweli.

“Lakini Rama, mbona huishiwi manjonjo na hauishi hamu kabisa baba,” Vivian alianza kuropoka huku akipeleka mikono kifuani kwa mwanaume huyo kama anayefanya zoezi la kudarizi kitambaa cha sare za wacheza shoo wa harusini!

Rama alizidi kupagawa kupindukia. Wingi wa kimiminika kichwani ukichanganya na ujuzi wa Vivian, mvulana huyo alikaribia kuyataja majina yote ya babu zake waliotangulia mbele ya haki miaka mia moja iliyopita.

Siku hiyo Vivian alipania ile mbaya kumaliza ufundi wote kwa Rama wake, mwanaume wa kwanza kabisa kumtoa ushamba alingia jiji la maraha, Dar es Salaam.

“Jamani Rama… Rama…. Ramaaaaa…,” Vivian alilama na kwa safari hii alipaza sauti kwa kiwango cha kuhamasisha zaidi. Akapeleka mikono yake na kumnyonyoa manyoya Rama na kisha kumalizia kwake na sekunde chache baadaye walibaki saresare maua wakibembea kwenye ulimwengu wa wachache, ulimwengu ambao hauna lugha thabiti ya kuelezea ikaeleweka zaidi ya kubakie kwenye hisia za akili na roho ya mhusika!

Walipashana na wote wakapashika. Mwanaume wa watu akajiweka sawa na kuingia kazini. Weee, achana kabisa na kinywaji alichokuwa amekipitisha kwenye koo yake Rama. Alichimbua mtaro hadi Vivian akalazimika kutumia nguvu kumuondoa kwenye mfereji wa maji taka. Kama ni mechi ilikuwa kali zaidi ya ile ya ngao ya hisani ya watani wa jadi.

“Basi inatosha mume wangu, nakupenda sana Rama jamani, kabisa baba yangu na kuanzia leo nakukabidhi maisha yangu yote. Wewe ndiye mwanaume unayefaa kunichukua jumlajumla. Kweli tena jamani, wala sitanii naapa mimi weeee,” Vivian alikiona cha mtemakuni.

Mchezo ulichezeka na kuhitimika kwa timu zote mbili kutoa suluhu ya mabao mawili kwa mawili. Wote walikuwa hoi na kutoka mioyoni mwao, kila mmoja alikiri na kujisikia hali ya kumkubali mwenzake.

“Lakini Rama, hakika wewe ni kiboko baba yangu,” Vivian alisema huku akimuegemea Rama kifuani kwake, lakini kabla Rama hajajibu chochote, ghafla mlango uligongwa na kwa kuwa Vivian ndiye alikuwa mwenyeji alivaa taulo harakahakara na kutoka kuufuata mlango ambapo alifungua taratibu na wakati anajiandaa kuuliza ni nani mgongaji, alishtukia akisukumwa na kuanguka hadi chini, kufumba na kufumbua alikuwa ni yule mjumbe wa nyumba kumi akiwa ameambatana na Jisu, yule fundi ambaye alimtengeeneza mlango Vivian wakati ule wa ugomvi wake na mzazi mwenzake ambapo baadaye walizaa penzi kutokana na kuzidiwa na pombe.

Mjumbe na Jisu walidhamiria kufanya fujo ya aina yake kwa Vivian. Walijitosa ndani na kuanza kurusha vitu huku na kule. Kifupi ni kwamba walikuwa wamelewa kupindukia. Rama alishtuka si kitoto. Alichokumbuka kukimbilia ni kuvaa nguo na kusimama kiume.

Kiasili Rama alikuwa mwanaume shupavu na kwa historia fupi ni kwamba aliwahi kujiunga na jeshi lakini hakumalizia mafunzo kutokana na kuugua ghafla kwa muda mrefu hali iliyopelekea kuachana na jeshi, kwa hiyo alikuwa vizuri sana lilipokuja suala la kurusha makonde.

Kichwani alikumbuka maelezo ya Vivian kwamba kwa wakati huo hakuwa na mwanaume hivyo Rama alijawa na ujasiri mkubwa, ingawa ukweli ni kwamba Vivian alikuwa mwanamke zoazoa. Kila mwanaume alikuwa wake, inategemeana tu na gia atakayomuingilia.

“Vivian hawa ni akina nani mama?” Rama aliuliza huku akijaribu kumzuia mjumbe na Jisu wasiendelee kufanya fujo mle ndani.

“Ni miongoni mwa wanaume wanaonisumbua mtaani hapa kimapenzi lakini mimi nimekuwa nikiwakatalia na leo wameamua kuja kunifanyia fujo…,” Vivian hakumalizia maelezo yake, Rama aliamua kuingia kazini. Aliwakusanya wote na kuwapigisha vichwa ambavyo si vya mkoa wala nchi hii.

Walipigika ile mbaya na kisha kuwatoa nje ambapo soo lilikuwa kubwa na kukusanya mtaa mzima.

Mjumbe ambaye alikuwa akiogopeka mtaani hapo kwa ubabe na ukorofi, sasa alikuwa mkononi mwa Rama akichezea kichapo kitakatifu tena mbele ya wananchi wake na hakuna aliyethubutu kuamulia zaidi ya kushangilia na kuuliza kulikoni na walipobaini kwamba chanzo kilikuwa ni kumfanyia fujo Vivian, walizidisha makelele.

Ni kama Mungu, wakati vurumai hiyo ikiendeela, gari la polisi ambalo lilikuwa doria maalum lilifika maeneo yale na kuwachukua wahusika wote, yaani Vivian, mjumbe, Jisu na Rama na kwenda nao kituo cha polisi ambacho hakikuwa mbali kutoka hapo. Walilazwa mahabusu hadi kesho yake asubuhi ambapo kulingana na maelezo yao, Rama na Vivian waliachiwa huru na kuwaacha mjumbe na Jisu kwa mahojiano zaidi ambapo askari mmoja aliambatana na Vivian hadi nyumbani kwake kwa ajili ya kufanya tathmini ya vitu vilivyoharibika kutokana na ugomvi huo.

Siku chache baadaye, Vivian na Rama walikubaliana kuoana na kwa kuwa Rama alikuwa na dini tofauti na Vivian kwa pamoja walikubaliana kufungia ndoa bomani na Vivian aliamua kuacha kazi mwenyewe kwenye ile Kampuni ya Nta na Asali na wakaamua kufungua biashara zao huku wakimtumikia Mungu kila mmoja kwa imani yake na ndoa yao ikishamiri kwa furaha na raha mstarehe, ambapo Vivian aliamua kukiri dhambi zake zote kanisani kwake.

Kwa upande wa Bigambo naye aliachana na maisha ya kuzoazoa wanawake hovyo na aliokoka na kuanza kumtumikia Mungu kwa kwenda kanisani na kushiriki ibada mbalimbali, ilifikia kipindi akakutana na Vivian akiwa na Rama katika majukwaa ya dini, wakawa waumini wazuri ambapo sasa walianza kuitana kaka na dada na maisha yalibadilika kabisa.

Kwa upande wa Jisu na mjumbe walihukumiwa kifungo cha miezi sita jela kwa kushindwa kulipa faini na fidia kwa uharibifu baadhi ya vitu vya Vivian na walipoachiwa wote waliokoa na kuachana kabisa na maisha ya kijinga na cha kushangaza wote waliamua nao kumtumikia Mungu, ikawa familia yenye upendo na maisha yao yakatawaliwa na Mungu na hadi sasa walishabadili kabisa maisha na kila mmoja wao anafurahia uwepo wake duniani.

MWISHO..

KUTOKA KWA MWANDISHI

Katikati ya chombezo hili kulikuwa na changamoto za hapa na pale ambazo wasomaji mlituma SMS zenu na kueleza maoni yenu. Asanteni kwa kuwa pamoja kuanzia mwanzo hadi leo tunapoahitimisha chombezo hili tamu kabisa ambalo naamini limekuacha na funzo kubwa maishani mwako. Maisha yanabadilika jamani. Usikose kufuatilia chombezo jipya kabisa siku ya Jumatano ijayo kwenye Gazeti la Risasi Mchanganyiko.

Kwa maoni na ushauri nicheki kwa namba hizi; 0679 65 96 33.

Comments are closed.