Jamani Antiii…Nishushe Ununio-16
ILIPOISHIA RISASI JUMAMOSI…
“Mwanzoni sikutaka kwa kweli, lakini ushawishi wako umesaidia sana hadi nikajikuta nafurahia maandalizi na hatimaye namna ambavyo mchezo mzima ulivyokwenda,” Vivian alisema na hapohapo akawa anamalizia zoezi la kuvaa na kumsubiri Bigambo amalize ili waweze kutoka pamoja kabla ya kuachana na kila mmoja kuangalia njia na ratiba yake.
TAMBAA NAYO SASA…
BIGAMBO alikuwa tayari ameshavaa suruali yake na muda huu alikuwa akivaa shati. Upande wa Vivian ndiyo kwanza alikuwa akijivuta katika kuvaa nguo…mara achukue sidiria na kuigeuza mara aiweke sawa…
“Vipi nitangulie?”
“Hapana bwana kwa nini uniache Bigambo wakati kuingia tumekuja wote… mechi tumecheza wote tena kwa furaha ya juu kila mmoja amefurahi kufika kileleni…”
Bigambo alionekana kukasirika licha ya kuambiwa maneno mazuri ya kuliwaza na Vivian…
“Unavaa taratibu sana lakini…mbona kabla hatujaanza kucheza mechi ulikuwa unavua harakaharaka?” Bigambo alimtania Vivian akaonesha tabasamu na kuvaa kwa spidi…
“Haya nimemaliza… kifuatacho?”
“Tuachane hapo nje mi niende kazini na wewe uendelee na ratiba zako,” alisema Bigambo na Vivian kukubali kwa kutikisa kichwa.
Walitoka nje kama walivyokuwa wameahidiana… Vivian akielekea nyumbani kwake ambapo alikuwa na ahadi ya kukutana na rafiki yake mwingine ambaye Bigambo hakuwa akimjua.
***
“Nimekusubiri sana… nakupigia simu yako hupokei kwa nini jamani?” Rama alilalamika mara baada ya Vivian kufika karibu na nyumbani kwake na kumkuta akiwa nje.
“Nisamehe si unajua tena Kariakoo kulivyokuwa na mavurugu…simu nilikuwa naisikia sana lakini ilikuwa kwenye pochi nikasema nikifika ndiyo nitaangalia nani alikuwa amepiga,” alijitetea Vivian.
Rama na Vivian waliwahi kuwa wapenzi kipindi cha nyuma ambacho Vivian alikuwa akiingia rasmi kwenye usichana wake…mapenzi yao yalikuwa ya kukorofishana na kurudiana. Kipindi hiki walikuwa hawajaonana karibia miezi sita na Rama ndiye aliyeanza kumtafuta na kukubaliana wakutane nyumbani kwake na kumpa maelekezo hadi nyumba anayoishi.
“Basi nisamehe mimi ambaye sikuwa najua ulikuwa katika wakati gani?” Rama naye alitupia jiwe gizani ili kumlegeza Vivian aliyeanza kuonesha kama mtu aliyekasirika. Rama ni kati ya wanaume waliokuwa wakimjulia sana Vivian pale anapokuwa amebadilika jinsi gani ya kumuingia.
“Nimefika hapa nje kama ulivyokuwa umenielekeza lakini bado sijajua hata ni nyumba ipi zaidi ya kuniambia nikifika nitakuta kwa nje kuna duka limeandikwa Massawe.”
“Akili zako za darasani kumbe bado zinafanya kazi vizuri. Duka la Massawe hilo hapo na kwangu paleee,” Vivian alimuelekeza Rama kwa alama ya kunyoosha kwa mkono.
“Tungetafuta sehemu basi tuongee tupate kidogo,” Rama alitupia swali la kiuchokozi.
“Huko nilipotoka nimezibwia za kutosha si unaona ninavyoyumba kwa mbali…”
“Basi tutafute sehemu tuongee.”
“Ni sawa lakini kwangu kunatosha wala usiogope!”
“Hapana, kuna kipindi uliniambia umeshapata mtu kwa hiyo naogopa kufumaniwa,” alisema Rama akionesha tabasamu mbele ya kope za Vivian.
“Haaa haaa Rama bwana! Akupige nani kwa maisha haya ya siku hizi?”
“Si bwana wako unayeishi naye?”
“Sikiliza Rama! Siku hizi nimekuwa tofauti kwanza nawachukia kweli wanaume, pili natamani hata ningekuwa mwanaume tu,” Alisema Vivian kwa msisitizo.
“Hapana Vivian usiseme hivyo! Ujue umeumbwa hivyo mwanamke, ni kosa kumsema vibaya aliyekuumba hata katika maandiko ipo hiyo,” Rama alidakia na kumfanya Vivian kumuelewa.
“Haya twende ukapafahamu ninapoishi,” Alisema Vivian na kusababisha furaha ndani ya moyo wa Rama aliyekuwa amelimisi penzi la Vivian kwa zaidi ya miezi sita na hata ujio wake ulikuwa kujaribu tu.
“Tangulia mbele mi nakuja kwa nyuma.”
“Haaa haaaa Rama bwana! Haya twende!”
Waliongozana hadi kwenye mlango wa Vivian. Vivian alifungua mlango wake na kutangulia ndani…akawasha taa kufanya nyumba iwe na mwanga mara mbili yake.
“Sasa unaweza kuingia ndani,” Vivian alimwambia Rama huku akishusha pazia vizuri. Rama akazama hadi ndani na kujitupia kwenye kochi.
“Umejipanga? Safi sana!” Alisema Rama kiuchokozi.
“Nijipange wapi? Mjini hapa nikasema nisikae kihasara japo vijikochi na TV na hako kagesi vinatosha!” Alisema Vivian akimwangalia Rama kana kwamba kuna kitu anataka kumuuliza.
“Hujaniambia, wifi anaendeleaje huko? Vipi una watoto wangapi sasa hivi?” Vivian alirusha swali kwa Rama.
“Watoto nitoe wapi wakati bado nataka kula ujana! Nipo singo kwa sasa!”
“Heee! Rama jamani kwa nini?”
“Basi tu si unajua maisha, ujue kuna wanawake wengine wameumbwa tofauti sana,” Rama aliinuka mahali alipokuwa amekaa na kushuka chini kabisa kwenye kapeti ambapo Vivian alikuwa amekaa.
“Huwezi amini kwa sasa nimeamua nijikite tu katika biashara zangu mikoani, ukifika muda wa kuishi na mwanamke nitaishi naye lakini si kwa sasa!”
“Bado sijakuelewa vizuri, yule wifi yangu wa kipindi kile ulichonitambulisha sijui alikuwa akiitwa Anna yupo wapi kwa sasa?” Vivian aliendelea kumkazia Rama.
“Ndiyo huyo niliyeachana naye baada ya kurudi safari na kukuta amesafisha karibu chumba kizima na kuniachia kapeti tu na kitanda chumbani…” alisema Rama kana kwamba ni kweli kumbe alikuwa akicheza na akili ya Vivian bila kujua.
“Masikini pole sana, pole…” Vivian alijikuta akiingiwa na moyo wa huruma…alichukua mkono wake na kumgusa Rama begani…Rama naye hakutaka kusubiri kuambiwa kitu, aliushikilia mkono mmoja wa Vivian.
“Asante sana Vivian…juzi uliponipigia simu sikutaka kuamini kama ni Vivian yule tuliyeanza naye uhusiano. Nikasema nisisafiri mpaka nije kukujulia hali kwanza na kukuona. Hivi namba yangu uliipata wapi maana nilibadilisha simu na namba ya simu hapa katikati,” Rama aliongea kwa sauti ya taratibu yenye kuliwaza masikio ya Vivian.
“Kama ulivyokuwa wewe, nilikukumbuka tu baada ya kukutana na rafiki yetu mmoja tuliyesoma naye si unamjua Maulanga?”
“Anhaaa kumbe ulikutana na Maulanga?”
“Yaaas! Ndiyo huyohuyo. Mgeni unatumia kinywaji gani maana naona maongezi yamekuwa mengi hadi nimesahau koo lako masikini.”
“Mhh! Vivian bwana! Asante situmii chochote.”
“Bwana Rama, chochote basi hata soda!” Alisema Vivian akiinuka na kuelekea kwenye friji lake lililokuwa limesheheni pombe kali mchanganyiko na soda.
“Nipe hiyooo…nimiminie kidogo kwenye glasi,” alisema Rama mara baada ya Vivian kufungua friji na kuona kinywaji aina ya Amarula.
“Umeniambia huna mtu sasa hii ukinywa si matatizo jamani?”
“Hakuna kitu kama hicho, watu wanaongeaga tu mbona hicho ni kinywaji kama vingine, hakileti kitu chochote mwilini.”
“Kukumiminia nakumiminia lakini tambua siku hizi mapenzi nooo!”
“Wala usijali,” Rama alimtoa wasiwasi Vivian…akamiminiwa kile kinywaji na kuanza kuinywa.
“Unaisikiaje?” Vivian alirusha dongo…ukweli ni kwamba hakutaka kucheza mechi yoyote na Rama kwa kuwa Bigambo alikuwa amemaliza kiu yake yote. Ile kauli yake ya kuachana na wanaume ambao walikuwa wakimtumia tu ilikuwa imeendelea kukaa katika kichwa chake.
“Naisikia murua kabisa! Hizi huwa nakunywaga mara mojamoja nikiwa safarini, huwa zinachangamsha mwili sana,” Rama alianza kuongea maneno mengi baada ya kukata fundo tatu za fasta.
“Mi nimeiweka tu kwa wageni na pia nikitaka kumleta mpenzi wangu huwa naanza kutumia hiyo kwanza.”
“Kumbe una mpenzi?”
“Kwa umri huu kweli Rama nikose mpenzi?”
“Umekuwa msiri sana Vivian ila hongera sana!” Rama alionesha kukata tamaa kwa kile kilichokuwa kimeanza kujengeka kichwani mwake juu ya kumvaa Vivian na kesho yake asafiri kufanya biashara zake.
“Hongera sana!” Rama alitua glasi yake chini na kumshika Vivian mikono yake yote miwili.
“Asante Rama, asante sana!”
“Nina ombi moja tu kwako kabla hata sijaondoka,” Rama alitupia swali kwa Vivian.
“Niambie tu nipo tayari kukusaidia.”
“Vivian wewe ni kati ya wasichana warembo wenye kumvutia kila mwanaume! Umeumbwa ukaumbika mamaaa! Nakuomba kwa muda huu tukumbushie yale mambo yetu ya zamani kipindi kile tumeanza uhusiano,” Rama kwa mara ya kwanza alishindwa kuzuia hisia zake na kujikuta akishikilia mapaja ya Vivian… Vivian akajitahidi kuepukana naye lakini akashindwa kwa sababu kile kinywaji kilimtuma Rama kuhama eneo la mapaja na kuelekea katika kifua cha Vivian hali iliyomfanya kuwa mpole na kumuacha akiendelea kutazama idara nyeti…
Je, nini kitaendelea? Usikose mwendelezo wa chombezo hili tamu katika Gazeti la Risasi Jumamosi.
Comments are closed.