The House of Favourite Newspapers

Jamani Antiii…Nishushe Ununio-2

0

ILIPOISHIA KWENYE RISASI JUMAMOSI:

Wakati akijiandaa kusema alichokuwa amekusudia, ghafla Jagadi alitokeza na kuwatazama wote wawili kwa jicho la ‘duh mara hii mmeshakuwa na ukaribu huo’.

TEREZA NAYO SASA…

WOTE walishtuka. Vivian akamtazama Bigambo usoni kisha akayarudisha kwa Jagadi aliyekuwa bado anawatazama kwa zamu. Lakini hakuacha kutoa tabasamu. Alichofanya Bigambo ni kuendelea na ratiba zingine. Akawa anakagua chupa za asali kabla ya kikao cha kujadili ubora wa asali ya siku hiyo.

“Huyu mbona ametuangalia sana?” Vivian alimuuliza Bigambo huku akiachia tabasamu lake lenye kusahaulisha kabisa adha za foleni za asubuhi.

“Sijui, labda ana mambo yake,” Bigambo alijibu lakini moyoni aliujua ukweli kwa nini Jagadi aliwatazama kwa jicho lile.

“Watu wana mambo ya Kiswahiliswahili, huwezi kuwatazama watu kwa jicho la hivyo,”Vivian alisema na kuendelea na zoezi lake la kutazama asali huku mazungumzo yakiendelea.

Muda wa kikao uliwadia na watu wote walijumuika pamoja kwenye meza kubwa na ya kisasa kabisa, tayari kwa kujadili bidhaa ya siku hiyo. Mwenyekiti wa siku hiyo aliitisha kikao na wajumbe wakawa tayari. Vivian na Bigambo walikaa pamoja, lakini macho ya wajumbe wengi wakiwa wanaume hayakubanduka kwa wawili hao.

Kikao kiliendeshwa haraka na shughuli zingine zikaendelea. “utanitafuta baadaye tukutane kwa ajili ya kuzungumza,” Vivian alimwambia Bigambo ambaye hadi wakati huo walikuwa wamekolea kwenye urafiki mkubwa.

“Poapoa, nitakutafuta,” Bigambo alijibu haraka kisha kuendelea na majukumu yake, ambapo Vivian naye alitoka na kwenda kwenye mizunguko yake ya kusaka matangazo kwenye makampuni mbalimbali mjini.

Siku nzima Bigambo alishinda na furaha isiyoelezeka. Uzuri wa Vivian ulikuwa umetikisa kabisa ukuta wa ubongo wake, moyoni alitamani jioni ifike mapema ili awasiliane na Vivian kabla ya kukutana na kufanya naye mazungumzo ya kuupendezesha moyo.

Kazi zilifanyika. Hatimaye jioni ikawadia na Bigambo alimpigia simu Vivian ili kujua mahali alipokuwa.

“Ndiyo nimefika hapa River- Side, wewe uko kwa wapi?” Vivian alimuuliza Bigambo na kusikilizia jibu lake ili aone kama ataweza kumsubiri au atachelewa.

“Ndiyo najiandaa kutoka ofisini, lakini sitachelewa sana mama,” Bigambo alisema na kunyanyuka kitini kwake kwa ajili ya kujiandaa kuondoka.

“Mbona bado uko mbali sana na mimi nataka niwahi nikapike au tuonane kesho basi,” Vivian alijibu ingawa hakuwa na msimamo sana juu ya pendekezo lake la kuonana siku inayofuata.

“Hapana V, nafika sasa hivi mama kwani nitachukua bodaboda ili nikuwahi, sawa?” Bigambo alikoleza wakati akishuka ngazi za ofisini kuelekea chini tayari kwa kuchukua usafiri ili amuwahi Vivian.

“Basi jitahidi si unaona muda nao umesonga na hivi nilivyochoka na mizunguko ya leo ndiyo basi kabisa,” alichagiza Vivian kisha kukata simu.

Bigambo alitembea haraka hadi kuwafikia watu wa bodaboda na kuelewana na mmoja wao ampeleke River- Side. Dakika ishirini baadaye Bigambo alikuwa ameshafika River-Side.

Uko upande gani?” Bigambo aliuliza baada ya Vivian kupokea simu.

“Nimesimama kwenye hii stendi ya magari ya kwenda Makoka, hapa mwanzoni karibu na bucha, ukisogea utaniona nimesimama karibu kabisa na vijana wa bodaboda,” Vivian alisema.

“Okey, sikiliza…”

“Ndiyo.”

“Rudi nyuma kidogo.”

“Halafu.”

“Mkono wako wa kulia kuna baa moja inaitwa kwa Mama John, karibu tu na mahali uliposimama, utanikuta hapa.”

“Sawa,” Vivian alijibu na kuanza kurudi nyuma kama alivyoelekezwa na Bigambo.

Muda mfupi baada ya maelekezo hayo, Bigambo na Vivian walikuwa wamekaa meza moja wakitazamana kwa nyuso za furaha na uhuru wa nafsi.

“Nimechelewa?” Bigambo aliuliza japo moyoni aliamini kabisa kwamba swali lake halikuwa dhahiri kwani alitumia muda mfupi sana kutoka ofisini Sinza-Kumekucha hadi hapo River-Side.

“Wala,” Vivian alijibu kwa sauti ya chini na aibu za kikekike zikiutawala uso wake.

“Jamani karibuni,” ilikuwa ni sauti ya mhudumu akiwasikiliza kwa kinywaji.

“Mimi nipe Dompo na huyu nadhani Savanna au mama?” Bigambo aliagiza kwa mbwembwe kwani siku hiyo alikuwa vizuri mfukoni kutokana na posho ambayo huwa wanapewa kila wiki kazini kwao, alikuwa nayo, pia jioni ya siku hiyo alikutana na mkurugenzi mlangoni wakati anaingia ofisini na kupewa zaidi ya shilingi elfu 40 ikiwa ni pongezi kwa kufanya kazi nzuri sana jana yake.

“Sawa,” Vivian aliinama kuashiria kabisa kwamba Bigambo alikuwa ameotea aina ya kinywaji akipendacho.

Mhudumu aliondoka kufuata vinywaji.

“Bigambo bwana,” Vivian alisema bila kumalizia sentensi yake.

“Vipi tena Vivian?”

“Wewe mtundu sana jamani.”

“Kawaida mama.”

“Nikuulize kitu?”

“Uliza tu Vivian, sidhani kama kuna swali utauliza halafu nisiwe na majibu yake.

“Umejuaje kama napenda kunywa Savanna?”

“Nimeotea tu jamani, nimekosea?”

“Hapana, basi tu nimependa,” Vivian alisema na kuachia kicheko cha kukenua meno bila kutoa sauti.

Vinywaji vililetwa na kuwekwa mezani. Wateja wa jirani wakawa wanaitazama Dompo ya Bigambo kwa kuisindikiza kwa macho kabla haijatua mezani kwa wahusika.

“Karibuni jamani,” mhudumu aliwakaribisha kwa bashasha kubwa huku akifuta meza kwa uchangamfu mkubwa.

Vinywaji vilianza kunywewa na hadi wakati huo si Bigambo wala Vivian aliyefungua mdomo kumwambia mwenzake kwamba anamhitaji.

“Ila Bigambo wewe ni mwanaume wa tofauti sana,” Vivian alianzisha mazungumzo, tayari akiwa na Savanna tatu kichwani huku Bigambo akiwa ameshabugia glasi zaidi ya nne za kinywaji chake. Wote walishaanza kuchangamka kwa vileo.

“Kwa nini Vivian?”

“Mchangamfu na mtu unayejali sana,” Vivian alisema huku akimpa Bigambo mkono wa shukrani lakini kutokana na umbali uliokuwepo mkono ulipelea na kutaka kuanguka kutokana na kuegemea sana wakati wa kutoa mkono huo.

“Ooh, pole sana Vivian,” Bigambo alisema.

“Asante.”

“Sogea huku,” Bigambo alisema huku akiweka kiti kingine karibu kabisa na mahali alipokuwa amekaa na kumtaka Vivian akaribiane naye ili waweze kuongea kwa uhuru zaidi. Hilo halikuwa na kipingamizi na Vivian alilitii mara moja ambapo sasa walikaa kwa ukaribu mkubwa ambao ilikuwa rahisi kwa kugusana kwa wakati wowote na mahali popote.

“Unajua Vivian,” Bigambo alisema huku akipekea mkono wake wa kulia kwenye mapaja ya Vivian akitegemea pengine atakutana na upinzani mkubwa lakini hali haikuwa hivyo na badala yake Vivian alitulia kama anayesikilizia jambo.

Bigambo kuona hivyo, akazidisha mbwembwe ambapo sasa alianza kuutembeza mkono kwenye mapaja ya Vivian kwa mikogo na mtindo wa kutekenya, hali ambayo ilimfanya Vivian kufumbafumba macho na kuweweseka kwa uwazi kabisa huku naye akijisogeza zaidi kwa Bigambo. Vivian hakukomea hapo, naye alianza utundu wa kiaina kwa kumshika Bigambo maeneo ambayo yalimfanya adate.

Vinywaji viliendelea kunyweka. Bigambo alikuwa akikaribia kuimaliza Dompo na tayari kichwani walishaanza kuwa wawili.

“Vivian,” aliita Bigambo huku akimtazama usoni.

“Bee…”

“Nataka nikueleze ukweli kabisa kutoka moyoni.”

“Sema tu B.”

“Nataka tuingie ndani tukazungumze kwa uhuru maana macho ya watu.” Bigambo alisema na kushindwa kufunguka kwa uwazi.

“Jamani Bigambo huko ndani si ndiyo tutazaa na mengine?”

“Mengine kama yapi jamani?”

“Aaah, unajua bwana.”

“Hapana, hatuwezi kufanya chochote kwa leo zaidi ya kuwa na uhuru tu,” Bigambo alisema huku akizungusha mkono wake kiunoni kwa Vivian ambapo alijikuta akigusa vitu vigumu viamshavyo hisia za ndani kabisa za mwanaume yeyote rijali.

“Sa…saaawa Bigambo lakini tusifanye looo….loteee,” Vivian aliitikia kwa maneno ya kukatakata kwa maana ya kuzidiwa na vitu viwili ambavyo ni Savanna na kule kushikwa kiunoni na Bigambo.

Walinyanyuka na kuingia ndani ya baa hiyo ambapo kwa upande wa kushoto kulikuwa na gesti.

Walichukua chumba kimoja na kuzama ndani ambapo si Vivian wala Bigambo aliyekuwa na uwezo wa kujizuia kwa lolote.

“Bigambo,” Vivian aliita na kujiegemeza zaidi kifuani kwa Bigambo huku akihema kwa pupa ikiwa ni pamoja na kuendeleza utundu wake mwilini kwa Bigambo muda mfupi tu baada ya kuketi kitandani.

Kuona hivyo, Bigambo alijiweka sawa na kumgeukia Vivian. Akanyoosha mikono na kuyaparamia maembe mawili na kufanya kama anayabonyeza ili kuona kama yameiva na yanafaa kuliwa.

Vivian aliruka na kutoa kilio kilichomfanya Bigambo aangue kicheko cha nguvu.

Je, nini kitafuata? Usikose kufuatilia katika Risasi Jumamosi siku ya Jumamosi. 0673 42 38 45.

NA IRENE M. NDAUKA

Leave A Reply