The House of Favourite Newspapers

Jamani Bebi, Kiuno Kinakaza! – 01

BAADA ya Mwatumu kupewa mashuti na maneno makali na meneja wake, aliamua kuondoka kwa hasira hadi chumbani kwake na kuanza kulia.

Akiwa anaendelea kulia ghafla akakumbuka kuwa yule mwanaume atakuwa bado yuko chumbani, hajaondoka.

Kwa hasira na ghadhabu kubwa aliamua kumfuata haraka sana. Alitoka kwa mwendo wa haraka hadi kwenye kile chumba na kuingia bila kugonga mlango.

“Sasa ni nini hicho ulichonifanyia jamani wewe mwanaume!” Mwantumu aliongea kwa hasira ambazo zilionekana dhahiri.

“Kwani nimefanya nini tena!” Mwanaume huyo akabaki akishangaa kwani hakuwa anajua ni nini hasa ambacho Mwantumu alikuwa akikilalamikia.

“Hiki ni nini sasa ulichofanya, eeh! Ebu angalia hiki ni nini sasa jamani! Kama siyo kuaibishana huko.”

Mwantumu aliendelea kulalamika huku akimuonesha mwanaume ambaye alikuwa amejilaza kitandani akiwa kifua wazi huku kiunoni kajifunga taulo jeupe, trei ambayo huwa anaitumia kubebea vinywaji.

Mwanaume yule aliamka alipokuwa amejilaza ili aangalie kitu anachooneshwa na Mwantumu.

“Dah! Sasa hii imefikaje humo kwenye trei yako ya vinywaji?” alihoji yule mwanaume.

“Nikuulize wewe ambaye umeiweka humu? Mwantumu naye akamuuliza tena swali yule jamaa.

“Oooh! Nimekumbuka, itakuwa nilipovua nilitumbukiza kwenye trei kwa kujua ni dastibini ya kutunzia uchafu.”

“Sasa wewe umeona hii ni ya kutunzia uchafu wako.”

“Pole sana mpenzi wangu.”

“Nani mpenzi wako, huku umenidhalilisha.”

“Nimekudhalilishaje?”

“Mimi nilipomaliza mchezo na wewe nilichukua trei yangu na kwenda moja kwa moja kaunta kwa ajili ya kuchukua vinywaji ili nipeleke kwa mteja.”

“Ikawaje sasa?”

“Nimefika nimeweka trei juu ya kaunta ili meneja aniwekee vinywaji.”

“Mmh!”

“Mmh nini sasa!”

“Nakusikiliza.”

“Ile anaweka si ndiyo anaona hii mdude wako ukiwa ndani ya trei.

“Meneja akaniuliza. Mwantumu hii ni nini!”

“Nikiwa bado namshangaa meneja kwa swali lile akanielekeza ndani ya trei, ile kuchungulia, mamaaaaaa! Aibu , wewe mwanaume umenitia aibu sana.”

“Te te te te teeeeeeh ! Te te te te the!” Mwanaume yule alianza kucheka.

“Unaona sasa ulivyo na dharau!”

“Siyo kwamba ni dharau?”

“Unacheka nini sasa kama siyo kunidhalilisha kwa kusudi!”

“Mwantumu siyo kwamba ninacheka kwa kusudi ila hata mimi nimeshangaa sana, kwa kweli nilijua ni dastibini ndiyo maana nikatupia humo. Nimecheka ulivyoniambia kuwa umeenda nayo hadi kaunta kwa meneja.”

“Pole sana kwa hicho kilichotokea wangu.”

“Nimeaibika sana, yaani sitamani hata kwenda kaunta tena.”

“Duh!’ kwa hiyo kazi utafanyaje sasa kwa leo?”

“Ndo itabidi unilipe mshahara wa siku nzima ya leo ili nipumzike, wewe unadhani aibu hiyo nani anaiweza?”

Hela haikuwa shida kwa Mchuga alichofanya alimpa shilingi 30,000 ambazo zilikuwa ni zaidi ya mara nne ya mshahara aliokuwa akilipwa kwa siku.

Kwani malipo ya Mwantumu na wenzake mara nyingi yalitegemeana na idadi ya vinywaji alivyouza kwa siku husika.

Kama akiuza kuanzia kreti moja au zaidi basi siku hiyo anakuwa ameingiza pesa nyingi sana.

Kwa hiyo kitendo cha kupewa shilingi 30,000 na Mchuga kilimfanya ajione kauchinja sana kwani hata kama angekuwa amepata mchepuko haikuwa rahisi kumpa kiasi hicho cha pesa zaidi ya shilingi 15,000 hadi shilingi 20,000.

Basi siku nzima Mwantumu alishinda kwenye chumba cha Mchuga wakila raha. Penzi la Mwantumu lilimnogea sana siku hiyo Mchuga.

“Mwantumu wewe ni mwanamke mzuri sana.”

“Uzuri wangu nini?” Mwantumu akauliza kwa sauti kubwa iliyoonesha kuharibiwa na vilevi pamoja na kuongea kwa sauti kubwa kutokana na kazi ya baa ambapo muda mwingi kunakuwa na muziki unaopigwa kwa sauti ya juu zaidi.

“Kwani Mwantumu hujui wewe kama ni mwanamke mrembo sana, ebu angalia macho yako jamani! Rangi yako nzuri, kiuno kizuri unacho.”

“Wewe ebu huko, mimi hapa sijaja kusifiwa nimekuja kutafuta pesa,” Mwantumu alimjibu Mchuga huku kakaza uso akimaanisha kwa kile alichokizungumza.

“Sawa najua unatafuta pesa, kwani kukusifia ni vibaya jamani!”

“Fungua kwanza mkwanja mambo mengine baadaye bhana!”

Mchuga ambaye alikuwa ameanza kumuelewa Mwantumu akaanza kupata shaka sana kulingana na majibu na maongezi ya Mwatumu.

Kwanza alijiuliza kama aliweza kumpa shilingi 30,000 ili asiende kufanyakazi kwa ajili ya kuficha aibu ya kile kilichotokea kaunta akiwa na meneja wake.

Pamoja na kuserebuka naye bado tena anaomba pesa tena kwa mtindo ambao unaonesha kuwa atakuwa ni mwanamke ambaye anafanya biashara ya kuuza mwili wake. Na inawezekana akawa ni mwanamke ambaye ameishazoea biashara hiyo.

“Lakini mbona anaonekana ni binti mdogo sana aiseee!” Swali la ghafla likajiuliza ndani ya kichwa cha Mchuga.

Mwantumu alinyanyuka alipokuwa amekaa kitandani na kusogelea mlangoni kisha kutungua nguo zake za ndani ambazo alikuwa ameziweka pale na kuanza kuvaa bra kisha nguo zingine ili aondoke zake.

“Baby mbona sikuelewi tena?”

“Hunielewi nini tena?”

“Mimi nilijua tunashinda wote mpenzi wangu.”

“Aka! Ushinde na nani, niache kwenda kutafuta hela ya kula nibaki nakufurahisha wewe tu.”

“Aha! Ukatafuteje tena hela ya kula wakati nishakupa ya siku nzima ili usiende kuabika, na sasa hivi umeniomba hela,” Mchuga alibaki akiduwaa kwa kauli na matendo na Mwantumu.

Akili ya Mchuga ilikuwa imezama hasa kwenye dimbwi la penzi nzito la msichana Mwantumu ambaye ni mfanyakazi wa baa moja maarufu ambayo imekuwa ikipokea wateja wengi sana kutokana na mmiliki wa baa hiyo kuwa anawaajiri wasichana wadogowadogo kwa ajili ya kufanya kazi ya kuhudumia huku akiamini kuwa wasichana hao ni mtego tosha kwa wanaume wakware wenye kupenda kuchepuka.

Mchuga alijitahidi sana kumbembeleza na kumweka karibu Mwantumu kwa sababu ya kumpenda kikwelikweli, lakini Mwantumu wala hakuwa na wazo hilo.

Akili yake ilitawaliwa na kutafuta pesa, hakuona shida kulala na wanaume hata watatu kwa kuwapa penzi la fastafasta.

“Mwantumu kuna jambo ambalo nataka kuzungumza na wewe?”

“Jambo gani hilo? Kama linahusu mkwanja haina shida.”

“Unamaanisha kama halihusiani na pesa basi nisikwambie?”

“Nilishaambiwa maneno mengi sana matupu, muda na zama hizo zilishapita kwa sasa ni kazi tu.”

Mchuga aliishiwa nguvu na kuamua kujitupa kitandani kwa nguvu na kisha akaanguka juu na kuanza kuwaza.

Je, Mchuga anawaza nini? Na nini anachokitaka kwa msichana Mwantumu. Usikose wiki ijayo.

Kwa ushauri na maoni tuma ujumbe (SMS) au WhatsApp kwa namba ya hapo juu, au nifollow kwenye Insta@ kungwimzoefu3080.

Irene Mwamfupe Ndauka

Comments are closed.