The House of Favourite Newspapers

Jamani faragha siyo usiku tu!-2

0

couple85620250Mpenzi msomaji, karibu kwenye kilinge chetu hiki kizuri cha XXLove ili tupeane ujuzi na elimu ya uhusiano wa kimapenzi.

Baada ya kujifunza muda wa kukutana faragha, leo nakualika tena katika mwendelezo wa mada yetu ya ‘Faragha Siyo Usiku Tu’ bali muda wowote pale mwenzi wako anapokuhitaji na wewe kuridhia na kuuruhusu mwili na akili yako kuhamishia kwenye tendo husika.

Leo nitazungumzia sehemu ya maswali ya wasomaji wa safu hii ambao walizungumza nami kwa njia mbalimbali. Mmoja wa wasomaji wangu aliniuliza: “Mpenzi wangu hataki faragha tuifanye muda ninaoutaka, nifanye nini? Naomba ushauri wako.”

Mpenzi msomaji na wengine wote wenye swali kama hilo, kwanza, nianze kwa kusema ni lazima kuwe na mambo kadhaa kati yako na mwenzi wako kabla ya kukutana faragha kwa muda unaoupenda.

couplesYAJUE MAJUKUMU YAKE
Kwa maisha ya sasa kila mtu ana majukumu yake. Haijalishi mnaishi pamoja au la! Yakupasa kujua majukumu ya kila siku ya mwenzi wako ili utakapomuhitaji basi utumie muda wake wa ziada au ule wa kupumzika. Kinyume cha hapo unakuwa haujatenda haki na kumlaumu mwenzako.

FANYA MAANDALIZI
Kila kitu huwa na maandalizi, kwa hiyo wakati unafikiria kukutana faragha na mpenzi wako ni lazima na yeye umuandae kwanza siyo kisa wewe umepata mhemko basi unataka tu bila kumuandaa mwenzako. Ukifanya hivyo unakuwa unakosea kwani faragha itakuwa ni ya wewe pekee kufurahi na si wote.

KUBALIANENI
Faragha nzuri ni ile ya wote wawili kukubaliana na ndipo tendo hilo hunoga na kuwa zuri kwani kila mtu anakuwa amejiweka tayari kukabiliana na mpenzi wake, lakini kama litakuwa siyo tendo la kukubaliana bali kulazimishana kwa nguvu ilimradi wewe umalize shida zako, basi ujue hakuna kitu ulichokifanya zaidi ya kumuachia mwenzako shombo na maumivu, jambo ambalo ni baya na linaweza kusababisha mpenzi wako kuwaza kukusaliti.
Kwa kifupi nilizungumzia suala zima la mazingira katika faragha muda mwingine tofauti na ule waliouzoea wengi.
Unaweza kuwa unatamani au unapenda kukutana na mwenzako muda huo kumbe mwenzio anakuwa amebanwa na kazi au majukumu mengine, aidha kukabiliwa na msongo wa mawazo kuhusu jambo f’lani. Tendo hili ni zuri kufanyika mkiwa mmejiandaa kiakili na kila kitu.
Tukutane wiki ijayo kwa mada nyingine motomoto. Pia usikose kutembelea ukurasa wetu wa
Mimi na Uhusiano kwenye Mtandao wa Facebook kujua mengi kuhusu mapenzi.

Leave A Reply