The House of Favourite Newspapers

Jamani Kaka Cheni …Ndiyo Nini Sasa?!-11

0

ILIPOISHIA WIKI ILIYOPITA:

“Hapana mama, niko macho.”

“Mbona kama hujatoka kuamka sasa hivi wewe, isijekuwa ulitoka ndiyo umerudi?”

“Hapana mama, nimeamka muda, nilikosa usingizi tu.”

“Kaka yako yupo chumbani kwake?”

TAMBAA NAYO…

“Sijajua mama.”

“Usiku alikuwepo?”

“Alikuwepo mpaka mimi nakwenda kulala.”

Mama aliufuata mlango wa chumbani kwa kaka Cheni, akaushika na kutikisa kitasa huku akiita…

“We Cheni…Cheni.”

Mimi miguu ilitetemeka, nusu nianguke. Najua kaka Cheni yuko chumbani kwangu tena chini ya kitanda, sasa itakuaje!

Mama alizungusha kitasa, mlango ukafungua huku akiendelea kuita…

“Wewe Cheni…Cheni…”

“Kama katoka itakuwa asubuhi hiihii mama, lakini mpaka anakwenda kulala usiku nilimsikia akifunga mlango,” nilisema mimi huku dhamira ikinisuta vilivyo.

Yaani mama ajue kaka Cheni yuko chumbani kwangu, sijui tutambebea mbeleko gani huyu mwanamke.

Aliachana na kaka Cheni akaingia ndani kwake. Kama nilivyosema, chumba changu na cha kaka Cheni vilikuwa uani na vilipakana. Chumba cha mama na vyumba vingine vilikuwa nyumba kubwa.

Niliingia haraka chumbani, nikainama kuangalia chini ya kitanda…

“Kaka, kama umeingia chumbani kwangu, toka haraka sana lisije likazuka balaa.”

“Wee sista, nisije nikatoka nikakumbana naye kwenye mlango?”

“Hamna bwana, toka chapuchapu! Nilikwambia mimi tangu majogoo yanawika hukusikia. Ona sasa!”

“Si wakati wa lawama huu sista, kwani si tulistarehe wote.”

“Mimi sizungumzii ushetani wetu, nazungumzia ubishi wako wa kukataa kuondoka mapema.”

Kaka Cheni alitoka, akasimama mlangoni…

“Ngoja nimwangalie kwanza,” nilimtahadharisha.

Niliingia nyumba kubwa hadi sebuleni na kubaini kwamba, mama yuko chumbani kwake. Nikatoka mbio.

Kufika chumbani kwangu nilimshika mkono kaka Cheni, nikamtoa haraka sana, akaingia chumbani kwake. Ile anafunga mlango tu, baba anaingia…

“Mungu wangu,” nilisema kwa sauti ya moyoni…

“Shikamoo baba…”

“Marhaba, umeamkaje?”

“Salama, poleni na msiba.”

“Tumepoa mama.”

Baba aliingia ndani nyumba kubwa. Baada ya kama dakika kumi akatoka akiwa ameongozana na mama…

“Kaka yako yuko?” aliuliza baba.

“Yupo.”

“Amerudi saa ngapi?” aliuliza mama…

“Anasema alikwenda kununua sabuni ya kuogea,” nilimtungia uongo…

“We Cheni,” aliita mama.”

“Naam.”

Kaka Cheni alikuja, lakini niligundua kwamba, nilimtungia uongo mbaya sana…

“Ulikwenda wapi?”

“Dukani…”

“Kununua nini?”

Mimi nilijua kaka Cheni alisikia niliposema alikwenda kununua sabuni, kumbe hakusikia…

“Kununua wembe,” alisema na kwenda kinyume kabisa na maelezo yangu…

“Wewe na dada yako nani muongo? Yeye amesema ulikwenda kununua sabuni ya kuogea, wewe unasema ulikwenda kununua wembe,” mama alikuja juu.

“Hata sabuni nilinunua mama,” alisema kaka Cheni.

Baba akadakia…

“Haya, kalete huo wembe na hiyo sabuni.”

Kaka Cheni alinikata jicho hilo, huku akiingia ndani kwake.

“Leo tunaumbuka, sijui kwa nini tumefanya mambo ya kijinga namna hii sisi, hakika tukio hili likipita salama naapa sitarudia tena na nitamheshimu kaka Cheni na kuogopa kuwa naye karibu,” niliwaza.

Baada ya muda kaka Cheni akatoka na sabuni ya kuogea ikiwa kwenye boksi jipya, mwenyewe nikashangaa…

“Huo wembe uko wapi?” aliuliza mama…

“Nimeupoteza.”

“Umeupotezaje wakati wewe ndiye uliyeununua?” mama alimwuliza kaka.

“Siyo nimeupoteza kwa maana ya kuuangusha, nimesahau nilipouweka mama,” kaka Cheni alijitetea.

“Ukisikia uzembe ndiyo huo, kwa mfano zingekuwa pesa si ingekuwa umepata hasara?” mama alimwuliza kaka.

“Ingekuwa hivyo mama, lakini siyo kwa kupenda,” kaka Cheni alimwambia mama aliyeishia kumwangalia tu.

Kifupi mimi nilijifunza kitu kwamba, maisha wanayotaka wazazi niyaishi mimi na kaka Cheni ni mabaya sana kuliko kutupa uhuru.

Kaka Cheni na ubwanga wake wote lakini anaambiwe asiwe anatoka nyumbani ni balaa!

***

Yaliisha, usiku ukaingia. Baba alikaa sana nje siku hiyo, najua alikuwa akimlenga kaka Cheni asitoke. Ilipofika saa sita usiku, baba akaingia ndani kulala.

Mimi nikamchokoza kaka Cheni kwa meseji…

“Dingi ndiyo kaingia, utatoka?”

“Kwenda wapi?”

“Si mademu zako.”

“Hata wewe demu wangu, njoo basi huku.”

Je, unajua nini kiliendelea huko? Usikose kusoma kwenye gazeti hilihili, wiki ijayo. 

Leave A Reply