The House of Favourite Newspapers
gunners X

Jamani Kaka Cheni …Ndiyo Nini Sasa?!-2

0

ILIPOISHIA WIKI ILIYOPITA:
Palepale kaka Cheni akanawa maji, akasimama ili aondoke…
“Cheni,” aliita baba…
“Naam…”

“Kaa hapo,” baba alisema kwa sauti yenye mamlaka. Kaka Cheni akakaa…
“Mimi nani?”
“Baba…”
SONGA NAYO MWENYEWE…

“Sasa unapata wapi ujasiri wa kunawa kabla yangu na kuondoka?”
Kikwetu, kama unakula na mkubwa, hata kama utatangulia kushiba huwezi kunawa. Itabidi chakula kwenye mikono kigandiane weee mpaka mkubwa ashibe, anawe yeye. Au kama vipi utoke ukanawie uani huko.

Lakini hilo linatokana na utamaduni wa kizamani kwani mtindo wa kunawa ni ule wa chombo kimoja. Anaanza mkubwa kuliko wote, anaingiza mkono kwenye chombo cha maji, akimaliza anakuja mkubwa anayefuatia mpaka mtu wa mwisho kuzaliwa.

Basi, kaka Cheni akaomba msamaha lakini bahati njema alikubaliwa msamaha wake akatakiwa kuondoka. Kaka Cheni aliondoka kwa kasi kama vile nje kulikuwa kuna basi lilikuwa linamsubiri yeye tu.

Nilijiuliza sana kuhusu hilo. Nikaunganisha na mlio wa mlango kufunguliwa, nikabaini kwamba, kuna mgeni kaka Cheni amemuwahi chumbani kwake na kama ni mgeni kweli, hakuna mwingine zaidi ya mmoja wa mademu zake kibao.

Tulimaliza kula, mimi nikatoa vyombo na kuviweka mahali kwake ili baadaye, chakula kikishashuka tumboni nianze kuosha.

Niliamua kwenda chumbani ili nikajilaze kidogo. Ile nafungua mlango tu, nikasikia sauti ya kike yenye mhemko kutoka chumbani kwa kaka Cheni. Mwanamke alikuwa akizungumza maneno matamu ya mapenzi huku akiweweseka kimahaba.

Licha ya mlango wangu kutoa mlio kuashiria kwamba naingia chumbani, lakini bado huyo demu hakuacha kupiga mayowe ya mahaba, tena aliongeza kasi.

Mwili ulinisisimka, nikahisi kibaridi kwa mbali huku nikiwa natamani nami nishikwe sehemu mbalimbali za mwili ili nijisikie nafuu. Hapo nilikuwa nimekaa kitandani kwangu.

Nilimsikia kaka Cheni akiguna kiume tu huku akiwa hasikiki anachosema lakini nilijua yupo katikati ya mechi na huyo mwanamke wake.

Mihemko ilichanganya, sasa nikawa nayasikia sawia maneno ya yule mwanamke. Alikuwa ananipa kwa sauti picha inayoendelea kule huku akimwamuru kaka Cheni mambo kadha wa kadha. Kama vile kuongeza kasi na kupunguza. Kuna wakati alimtaka kubadili mapozi.

Hali hiyo ilinipa mimi wakati mgumu sana kiasi kwamba nilijikuta napindukia kitandani na kulala chali kuangalia juu.

Licha ya jua la mchana kuwaka sana na kusababisha joto, lakini sikuona kama ni madhara kwangu. Niliendelea kufuatilia mpambano wa chumbani kwa kaka Cheni.
Kama vile haitoshi, nilianza kujishikashika mwenyewe sehemu mbalimbali za mwili wangu nikifika hadi kwenye kifua na kutalii hapo kwa muda nikijihamasisha na mikono kwenye nido zangu.

Ilibaki kidogo nilie kwa sauti hasa baada ya yule mwanamke kumtaja jina kaka Cheni na kumwambia hatua inayofuata kwake.

Nilijikuta na mimi nikijinyoosha miguu na kutulia tuli kwa muda huku nikihema kwa kasi. Sikujua nini kilitokea, nikapitiwa na usingizi mzito sana. Nilikuja kushtuka baada ya kuhisi mlango wangu unagongwa, nikakurupuka na kwenda kuufungua.
“Wewe utaosha vyombo saa ngapi?” mama aliniuliza.

“Nakwenda mama.”
Kabla sijakwenda kuosha vyombo, nilikwenda kuoga kwanza. Si mnajua tena!
***
Siku hiyo baada ya chakula cha usiku, nilitoka zangu kwenda kwa jamaa yangu. Niliona afadhali akanikate kiu ili nikirudi, hata kama kaka Cheni atakuja na mmoja kati ya mademu zake, nisiwe na muhemuhe!

Nilimkuta jamaa yangu, akanipokea, akanipa mahaba nitoe uhai. Mambo yalikwenda vizuri sana. Saa nne usiku alinisindikiza kurudi nyumbani huku moyoni nikimcheka kaka Cheni kwamba kama lengo lake ni kunirusha roho mimi dada yake, aandike ameumia kwani mwenzake nilirudi nikiwa mwepesiii!

Nilipokaribia nyumbani, jamaa yangu aliniaga, akarudi kwake. Lakini ile naingia ndani tu, jamaa yangu akanitumia meseji kuniambia kwamba, amepishana na bro wangu Cheni akiwa na demu ana wowowo hilo, we acha tu. Nikamuuliza anakwenda wapi, hata kabla hajajibu, kaka Cheni akaingia chumbani kwake…

“Karibu Kibibi,” kaka Cheni alikaribisha, moyoni nikasema ohoooo! Kibibi namfahamu sana, si mwanamke bali ni shangingi asiyetaka kustaafu!

Ni kweli Kibibi ana liwowowo mfano mtaani kwenu hakuna! Mbaya zaidi anapenda sana kuvaa mikanga bila kufuli kwa ndani, sasa akitembea weee! Mbengele… mbengele…utasema kuna sehemu za nyama kwenye muwowowo wake zinakaribia kuanguka.

“Mmmh…kama ni Kibibi leo silali humu ndani,” nilisema moyoni kwani najua Kibibi ni mwanamke asiye na haya wala soni achilia mbali aibu.

Moyoni nilimsifu kaka Cheni, yaani mchana yule, usiku huyu tena! Loo! Niliamua kulala mapema ili nisisumbuliwe na mambo yao yatakapoanza. Niliwakadiria wataanza mechi baada ya kama nusu saa za kusaka stimu kwanza kwa maongezi, kumbe weee..!

Je, unajua nini kiliendelea huko? Usikose kusoma kwenye gazeti hilihili, wiki ijayo.

Leave A Reply