The House of Favourite Newspapers

Jamaniee! mnaisoma namba ndo kwanza siku 33

0

2015-10-30T122712Z_1541519139_GF20000038928_RTRMADP_3_TANZANIA-ELECTION_0_0 (1)Rais Dk. John Pombe Magufuli ‘JPM’.

Mwandishi wetu
WANAISOMA namba! Ni siku 33 tu (leo), tangu Rais Dk. John Pombe Magufuli ‘JPM’ akabidhiwe Ikulu ya Magogoni, Dar, tayari mtetemeko mkubwa umetokea kufuatia agizo lake la kuitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuhakikisha inakusanya mapato ili nchi ijiendeshe akishadadia na msemo wake wa ‘Hapa Kazi Tu’.

Mbali na TRA, agizo la Rais Magufuli lilifika hadi Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) ambao wanafanya kazi kwa ukaribu na TRA hususan katika eneo la utoaji wa bidhaa bandarini.

KAZI IMEANZA
Agizo hilo limesababisha baadhi ya wafanyakazi wa TRA na TPA kupandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar kwa kile kilichodaiwa kuwa walihusika kwa namna moja au nyingine upotevu wa makontena 329 yalibainika kutoweka bandarini bila kulipiwa kodi.
Rais-Magufuli-9

Alipotembelea Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

WAZIRI MKUU AKOLEZA KASI
Kasi ya Rais Magufuli imeonekana kukolezwa zaidi na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa kufanya ziara mbili za kushtukiza pale TPA na Shirika la Reli Tanzania (TRL) ambapo alibaini utafunwaji wa mabilioni ya fedha za umma usiokuwa na maelezo ya kutosha.

BILIONI 90 ZIKO SERIKALINI
Lakini kwa upande wake, Rais Magufuli inaelezwa kuwa, katika siku zake za kuwepo madarakani tangu aapishwe kuwa Rais wa Tanzania, ameshaokoa wastani wa zaidi ya shilingi bilioni 90 kwa kufuta ziara za nje za maafisa wa serikali, kufuta sherehe za Uhuru za Desemba 9, mwaka huu na nyingine nyingi katika kuhakikisha pesa zinapatikana ili kuwatumikia Watanzania.

IMG_5434

…Alipotembelea hazina.

IJUMAA WIKIENDA MITAANI
Kwa siku tatu mfululizo, timu ya Ijumaa Wikienda ilizama mitaani jijini Dar ili kuzungumza na wasomaji wake kusikia maoni yao kuhusu kasi ya Magufuli ambayo imepamba moto nchi nzima, kwenye ofisi za serikali, hasa kwa watumishi wa umma wa kawaida na mabosi wao.

Baadhi ya wasomaji walisema kuwa, katika miaka mitano (siku 1825) ambayo ndiyo ya utawala wa rais kikatiba nchini Tanzania, Magufuli amesomeka kwa siku 35 tu tangu aingie ikulu. Kwa hiyo bado siku kibao na mambo makubwa yatafanyika.
“Huyu mtu (rais) ni kiboko. Mafisadi wanaisoma namba kwa muda mfupi sana. Rais wa Tanzania anatawala kwa miaka mitano ambayo ni sawa na siku 1825, yeye ameshatawala kwa siku 33.

“Kwa hiyo bado siku 1792. Je, akifikisha siku 365 ambazo ni mwaka mmoja? Si mafisadi watanyooka! Na hapo hana baraza la mawaziri. Mimi nataka watu wakaze buti, tutafika tu,” alisema Azaria Sanga, mkazi wa Kigamboni, Dar.

“Mimi nasikitishwa na watu ambao wameanza kuutumia msemo wa ‘kuisoma namba’ kwa ubaya. Kuna watu wanasema eti CCM (Chama Cha Mapinduzi) ndiyo wanaisoma namba wenyewe kwa sababu kasi ya Magufuli inawakumbuka wanachama wake. Hii si sahihi.

“Kama mtu una ufahamu utajua tu. Watumishi wa serikali wana vyama mbalimbali. Kasi ya Magufuli inamkumba kila mtu ambaye si mwadilifu,” alisema Zubeir Mhando, mkazi wa Kimara, Dar.

“Kwangu mimi Magufuli ametoa mwanga wa mwelekeo wa nchi kwa siku chache sana, naweza kusema ametawala nchi kwa wiki nne pengine, lakini ameshaokoa mabilioni ya pesa, unadhani akifikisha wiki kumi na mbili (miezi 3) itakuaje? Tumwombee jamani,” alisema mama Anolida, mkazi wa Buguruni, Dar.

Ijumaa iliyopita, maofisa nane wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), akiwemo Kamishna wa Forodha wa mamlaka hiyo, Tiagi Masamaki (56) wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kutoa makontena 329 bandarini bila ya kulipiwa kodi na kuisababishia serikali hasara ya shilingi bilioni 12.7.

Wengine waliopanda kizimbani ni Habibu Mponezya (45) Meneja wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja, Bulton Mponezya (51),

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Christopher Msigwa akisaidiana na Peter Vitalis. Watuhumiwa hao walikosa dhamana na kurudishwa rumande Gereza la Segerea, Dar.

Leave A Reply