The House of Favourite Newspapers

Jambazi Kambare Aliyeteleza Akikamatwa Auawa Dar – Video

JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limefanikiwa kuua watu wawili wanaodhaniwa kuwa ni majambazi sugu akiwemo aliyefahamika kwa jina la Kambare ambaye alikuwa akitafutwa kwa muda mrefu na jeshi hilo.

 

Hayo yamesemwa leo Jumatano, Novemba 6, 2019 na kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Lazaro Mambosasa wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelekea mkutano wa SADC unaotarajiwa kuanza keshokutwa, Novemba 8, katika Ukumbi wa Kimatataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

“Tunawashukuru Watanzania wanaendelea kutoa taarifa za uhalifu kwa Jeshi la Polisi, usiku wa kuamkia leo tumekamata pisto moja na majambazi wawili waliokuwa wakiwahangaisha wananchi wameangushwa chini (wameauawa). Mmoja ni aliyejiita Kambare, ametesa sana huko Madizini, Ukonga na maeneo mengine.

 

“Alikuwa na wenzake, wanakodi pikipiki, wanaielekezea sehemu aliko Kambare, wakifika pale Kambare anamchoma kisu au kumpiga risasi mwenye pikipiki kisha wanaichukua na kuondoka nayo. Amekuwa akiwateka na kuwaua madereva bodaboda, kila akikamatwa anateleza na kuwatoka askari, ndiyo maana akaitwa Kambare, lakini mwishowe na yeye ametangulia mbele za haki,” amesema Mambosasa.

 

Aisha, RPC Mambosasa amesema kuwa mgeni anapotapeliwa sifa inayobebwa ni ya watanzania wote na kuongeza kuwa tusikubali nchi ya Tanzania kuchafuliwa.

 

“Tumejipanga na doria zinaendelea mtaani, kikao cha SADC wageni wetu wanaoingia kuanzia Aairport, mahari watakapofikia na movement zao zote hadi kwenye kikao watakuwa salama. Fukwe zote na eneo la mkutano tumehakikisha usalama upo. Kila mmoja anatakiwa awe mlinzi wa mwenzake, wanaofanya ujanja ujanja toeni taarifa, tutawashughulikia, tusikubali mtu mmoja akachafua sifa ya nchi yetu,” amesema Mambosasa.

 

Na Edwin Lindege & Grace Khuni.

 

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Global Publishers (@globalpublishers) on

Comments are closed.