The House of Favourite Newspapers

Jambo Food Products waifanyia kazi kauli ya JPM – Video

KAULI mbiu y a Rais Dkt John Pombe Magufuli, ni Tanzania ya Viwanda! Malengo yake ni kuona viwanda vinajengwa kila kona ya nchi ili kuongeza uzalishaji mali, kutoa fursa za ajira kwa wazawa lakini pia kukuza uchumi wa nchi.

Kampuni ya Jambo Food Products, inaifanyia kazi kwa vitendo kauli mbiu ya mheshimiwa Rais Magufuli ambapo imefanikiwa kujenga kiwanda cha kisasa kinachozalisha vinywaji baridi zikiwemo soda, juisi, maji na kadhalika ambapo Rais Magufuli alikizindua rasmi, Januari 13, 2017.

 

Kizuri zaidi ni kwamba bidhaa zinazozalishwa na kiwanda hicho, zina ubora wa kimataifa na zimeonesha kufanya vyema zaidi katika soko la ushindani, huku umaarufu wa bidhaa zake ukizidi kuongezeka kila kukicha.

Miongoni mwa vinywaji vinavyozalishwa na Jambo Food Products, ni pamoja na Jambo Malta Lemon, Jambo Apple, Jambo Embe, Jambo Energy, Jambo Malta Pineapple, Jambo Lemon, Jambo Vito, Jambo Orange, Jambo Drinking Water na nyingine kibao!


 

Bidhaa zao zinapatikana nchi nzima kwa bei za jumla na rejareja na zimeonekana kuwa kimbilio la wengi kutokana na ubora wake pamoja na unafuu wa bei unaomfanya kila Mtanzania aweze kumudu kwa urahisi.

“Kwa kipindi ki refu mimi nimekuwa mtumiaji wa vinywaji baridi lakini tangu nilipoonja bidhaa za Jambo, kiukweli nimeiona tofauti na sitamani kutumia vinywaji vingine zaidi ya hivi vinavyozalishwa na Jambo Food Product,” alikaririwa Stumai Juma, mkazi wa Manzese jijini Dar es Salaam.

“Mimi ni mfanyabiashara wa vinywaji baridi, nauza vinywaji kutoka kampuni mbalimbali lakini kiukweli katika siku za hivi karibuni, wateja wengi zaidi wamekuwa wakivutiwa na bidhaa za Jambo, yaani mtu akionja tu lazima kesho arudi tena,” alisema Mwanaidi Sadick, mfanyabiashara wa vinywaji jijini Mwanza.

 

 

 

Jambo wanazalisha na kusambaza vinywaji hivyo kwa jumla na rejareja, vipo vinywaji aina ya; Jambo Malta Lemon, Jambo Apple, Jambo Embe, Jambo Energy, Jambo Malta Pineapple, Jambo Lemon, Jambo Vito, Jambo Orange, Jambo Drinking Water na nyingine kibaooooo!

 

Kiwanda cha Jambo kipo Shinyanga Mjini.
Simu: +255622666692 au +255622666680
Email: [email protected].

Website: https://jambogroup.co.tz

Stori: Waandishi Wetu, Dar

TAZAMA HAPA

Comments are closed.