Jamii Sports Club yaadhimisha Nyerere day kwa kuchangia damu
Wanajogging walioshiriki uchangiaji damu huo wakiwa katika picha ya pamoja.
Nyuso za furaha na hamasa tupu
Gazeti la Championi likisomwa na wanajogging.
Mmoja wa madaktari kutoka Hospitali ya Palestina akitoa ushauri nasaha kabla ya kutoa damu.
Madaktari wa Hospitali ya Palestina na Mwananyamala wakitoa huduma kwa wachangiaji damu salama.
Utoaji damu ukiendelea.
Daktari wa utoaji damu akimuandaa mwanajogging kwa ajili ya kutoa damu.
NA DENIS MTIMA/GPL
JAMII Sports Club yenye maskani yake Sinza jijini Dar, kwa kushirikiana na vilabu mbalimbali vya michezo vya jijini Dar, vimeungana na kuratibu bonanza la pamoja ikiwa ni njia ya kuadhimisha miaka 16 tangu kifo cha aliyekuwa Baba wa Taifa, Hayati Julius Kambarage Nyerere, ambapo pamoja na mambo mengine, vimeendesha zoezi la kuchangia damu.
Akizungumza na mwandishi wetu, wakati wa shughuli hiyo, mratibu wa mfuko wa uchangiaji damu uliofanyika kwenye kiwanja cha Shule ya Msingi Mashujaa jijini Dar, Henry Katabazi, amesema lengo la kujumuika na kuandaa bonanza hilo, ni kujenga uhusiano mwema, kujenga afya na kukumbuka mchango wa Mwalimu Nyerere kama mwasisi wa taifa letu.
Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa Manispaa ya kinondoni, Dk. Aziz Msuya, akizungumza na washiriki wa mabonanza hayo, amewapongeza kwa namna walivyoweza kujitolea katika uchangiaji damu salama na kusaidia wenye uhitaji huo na kwamba waendelee na moyo huo.
Baadhi ya vilabu vingine vya michezo vilivyoshiriki zoezi hilo ni pamoja na Mbagala Jogging , Mburahati Jogging , Tandale Jogging Ubungo Jogging Club na Msasani Jogging Club.