The House of Favourite Newspapers

Jamii Yawatenga… Kisa Kuiba Sanamu za Urithi

0

wachina wezi (3)Sanamu zilizoibiwa baada ya wezi hao kukamatwa.wachina wezi (5)Wezi wakitembezwa mitaani.wachina wezi (1) Sanamu zikirudiswa kijijiniwachina wezi (2)Wanakijiji wakizikagua sanamuwachina wezi (4)Wanakijiji wakipika na kufanya sherehe baada ya sanamu za urithi wa kijiji chao kurudi

KAMA kuna njia nyingine ya kuwakumbusha watu kutokuiba basi hii ni njia mbadala ambayo ikiigwa inaweza kusaidia kwa namna moja ama nyingine.

Watu watano wanaosadikiwa kuiba sanamu mbili za urithi kwenye mtaa wa Miaoba, Kijiji cha Tongzi, Jimbo la Guizhou, Kusini Magharibi mwa China wametengwa na jamii yao baada ya kukumbwa na mkasa huo Alhamisi iliyopita.

Mamia ya wanakijiji walikusanyika kwa pamoja kulaani kitendo hicho  cha vijana watano kuamua kuiba sanamu mbili za simba zilizochongwa kwa mawe.

Sanamu hizo ambazo yamebeba viashiria vya imani ya buddha zinakadiriwa kuwepo kwa zaidi ya miaka 400 iliyopita , ziliibiwa asubuhi ya Oktoba 13 mwaka jana.

Wanakijiji walita polisi ili kufanya uchunguzi kutokana na tukio hilo ikiwemo kubaini wezi na wausika wengine wa tukio hilo. Baadaye waligundua kuwa tukio hilo lilifanya na vijana wa magengeni kijiji hapo ndipo jitihada za kuwasaka zikaanza.

Wahusika watano wa tukio hilo walikamatwa Januari 27, ikiwa ni miezi mitatu baada ya wizi huo kutokea.

Wanakijiji wamedai kuwa sanamu hizo zimekuwa zikirithiwa kizazi na kizazi katika jiamii yaona kuleta baraka na neema nyingi kijijini hapo kutokana na mani yao.

Leave A Reply