The House of Favourite Newspapers

Jaqueline Mengi Kuwaongoza Mamiss Tanzania Kusherehekea Urembo

0
Mamiss hao kutoka kushoto, Genevieve Mpangala, Hapiness Magese, Jaquiline Mengi, Nancy Sumari na Queen Elizabeth Makune.

Miss Tanzania mwaka 2000 Jaqueline Mengi kwa kushirikiana na mamiss wenzake waliwahi kushika taji hilo wameanzisha mpango wa kuwahamasisha wasichana na wanawake kuchangisha fedha za kusaidia afya na elimu.

Hapiness Magese akizungumzia tukio hilo.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar leo Jaqueline amesema mpango unaoitwa Beauty Legacy 2020 utazinduliwa Novemba 14 mwaka huu kwenye Hoteli ya Hyatt Regency (Kilimanjaro Hotel) Jijini Dar es Salaam.

Nancy Sumari kwenye pozi baada ya hafla hiyo.

Hivyo ameyataka makampuni, watu binafsi na wengineo kujitokeza kufadhili shughuli hiyo ambayo itakwenda kuwasaidia watoto waliozaliwa kabla ya umri (njiti), kutoa miguu bandia kwa watu wanaishi na ulemavu, kufanya ukarabati wa wodi za wazazi na miradi mingine kama hiyo na kusaidia sekta ya elimu.

Wanahabari kazini.

Katika mkutano huo na wanahabari baadhi ya warembo waliohudhuria mkutano huo ni pamoja na Miss Tanzania 2018, Queen Elizabeth Makune, Miss Tanzania 2010 Genevieve Mpangala, Miss Tanzania 2005 Nancy Sumari, Miss Tanzania 2001 na Hapiness Magese.

Jaqueline Mengi akijibu maswali ya wanahabari hawapo pichani.

Jaqueline amesema mamiss waliowahi kutwaa taji hilo wanatarajiwa kuwepo kwenye uzinduzi huo wa Septemba 14 mwaka huu.

Hapiness Magese akifafanua jambo kwenye mkutano huo.                                                                                HABARI/PICHA: NA WAANDISHI WETU  
Leave A Reply