The House of Favourite Newspapers

Jaramba la Mwisho la AFC Leopards Kabla ya Kuwavaa Singida United

Kikosi cha AFC Leopards ya Kenya kimejifua mapema leo asubuhi kabla ya kukabiliana na Singida United katika mchezo wa SportPesa Super Cup kesho kwenye Uwanja wa Afraha mjini Nakuru.

Singida kutoka Tanzania itakuwa inacheza na Leopards baada ya Simba kukipiga na Kariobang Sharks leo saa 9 alasiri ambapo Mabingwa hao wa VPL wametinga nusu fainali ya kombe hilo baada ya kuinyuka Kariobang Sharks kwa jumla ya mikwaju ya penati 3-2.

Tazama pichaz za matukio ya mazoezi ya Leopards walivyojifua asubuhi ya leo.

PICHA NA MUSA MATEJA ALIYEKO KENYA

Comments are closed.