Jay Moe haoi, why? Kwa nini?
Msanii wa Bongo Fleva, Jay Moe.
Hamida Hassan
Msanii wa long time kwenye anga la Bongo Fleva, Jay Moe ameeleza sababu za kwa nini mpaka leo hajachukua jiko licha ya umri wake kwenda.
Kwanza anasema, mpaka sasa hana mchumba na suala la kuoa linamuwia vigumu kwa sasa kwani bado anamtafuta ambaye ataenda sawa na ndoto zake, siyo leo anaoa ilimradi anaoa halafu kesho ndoa inavunjika.