The House of Favourite Newspapers

Jay: Tusionane Wabaya!

MKONGWE kunako Bongo Fleva na Mbunge wa Mikumi, Joseph Haule ‘Jay’ amesema hakuna sababu ya wasanii kuonana wabaya, badala yake waungane na kushindana kwa kutoa ngoma kali ili kuupeleka muziki huu mbali zaidi.

 

Akizungumza na Ijumaa ShowBiz mara baada ya kuweka heshima kwenye Wasafi Festival, wikiendi iliyopita katika Viwanja vya Posta-Kijitonyama, Dar, Profesa Jay alisema, tofauti za wasanii zinasababisha Bongo Fleva ishindwe kufika mbali kutokana na chuki kati ya wasanii.

 

“Tusionane wabaya, tushindane, tusichukiane. Mabifu hayasogezi mbele muziki wetu. “Mfano Diamond na Kiba, natamani sana niingilie kati, lakini sijui chanzo,” alisema Jay ambaye anaamini Bongo Fleva sasa inafanya vizuri Afrika kiasi cha kutishia muziki wa Nigeria.

Comments are closed.