The House of Favourite Newspapers

Jay Z Na Beyonce Kununua Nyumba Ya Bei Ghali ($200 Million) Zaidi Jijini Los Angeles – (Video)

Kuwa superstar sometimes ni raha sana… why? Ukiwa kama Jay Z na Beyonce unakuwa na uwezo wa kununua kitu chochote kile upendacho ikiwemo nyumba ya bei ghali kuliko zote jijini Los Angeles nchini Marekani!

Good morning mdau, leo jumatatu ya March 6 2017 imenipeleka moja kwa moja mamtoni ambapo mtandao wa PEOPLE umeripoti kuwa weekend iliyopita The Carters walikuwa jijini Los Angeles wakitafuta nyumba ya kuanzia maisha mapya na kuvutiwa zaidi na nyumba ya bei kubwa kuliko zote jijini humo.

Nyumba hiyo yenye ukubwa wa mraba 57,000 inapatikana maeneo ya Holmby Hills ambapo awali ilikuwa inamilikiwa na Television Producer Aaron Speeling na mke wake Candy toka mwaka 1991. Baada ya kufariki kwa Aaron Spelling mwaka 2006 ambaye ndiye aliyeijenga nyumba hiyo, mkewe aliamua kuiweka nyumba hiyo sokoni kwa bei ya $150 Million lakini kufikia October mwaka 2016 nyumba hiyo ilikuwa inauzwa kwa bei ya $200 Million.

Ndani ya nyumba hiyo, kuna vitu mbalimbali ikiwemo maktaba ya kusomea, chumba kikubwa cha sinema, gym ya mazoezi, chumba cha midoli, studio ya kucheza mchezo wa bowling, hifadhi kubwa ya wine, vyumba vya kulala visivyo pungua sita, jiko sita, na bafu 26 . Mbali na vile vinavyopatikana ndani ya nyumba hiyo, nje ya nyumba hiyo kuna uwanja zaidi ya mmoja wa tennis, bustani yenye ukubwa wa ekari 5  pamoja na swimming pool.

Sources karibu na The Carters wanadai kuwa familia hiyo inataka kuhamia jijini LA moja kwa moja na wangependa kuimiliki nyumba hiyo haraka iwezekanavyo.

Itazame video ya nyumba hiyo hapa chini:

 

Imeandikwa Na: Sandra Brown.

Subscribe kwenye YouTube Chanel yetu ya Global TV Online ili zote kali zinazotufikia iwe ni siasa, michezo, comedy, burudani, muziki na nyingine zikufikie kwa wakati.

Comments are closed.