#GlobalCelebNews: Jay Z na Beyoncé Wana Utajiri Zaidi ya Dola Bn. 1

WANANDOA wawili wakali wa wanamuziki wa familia ya Carters, ambao ni Jay Z na Beyoncé wana mkwanja unaovuka Dola bilioni moja.

Kwa mujibu wa jarida la Forbes, Hov (Jay Z) ana ‘mpunga’ unaofikia Dola milioni 810 na mkewe, Yoncé, ana Dola milioni 350 na hivyo kuwafanya wanandoa hao kuwa na Dola bilioni 1.16 kibindoni.

Pamoja na habari hiyo, kivutio zaidi cha utajiri huo ni kwamba huenda takwimu hizo zilizotajwa si za sasa.  Takwimu za Jigga (Jay Z) zinatokana na listi ya watu watano  iliyotolewa na Forbes kabla hata ya ziara iliyomwingizia mwanamuziki huyo Dola 20 milioni alipozunguka sehemu mbalimbali  Marekani kutumbuiza.

Utajiri wa Jay Z unatokana na vyanzo mbalimbali ikiwa ni pamoja na shampeni ya Roc Nation and Armand de Brignac.  Wakati huohuo, Malkia Bey (Beyoncé) huingiza mkwanja kutokana na vyanzo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kufanya maonyesho ya peke yake na  biashara ya nguo kupitia kampuni za Ivy Park na Parkwood.

Nyota hao wawili pia wanamiliki kampuni la huduma za muziki la TIDAL  ambalo linazidi kushamiri kwa kushirikiana na lile la Sprint.

 

Wanandoa hao matajiri wanaotegemea kupata watoto mapacha hivi karibuni, wanasaka nyumba ya anasa itakayogharimu mamilioni ya Dola huko Los Angeles kwa ajili ya familia yao ambayo inazidi kupanuka.

Toa comment