Jay Z, Gaga Miongoni Mwa Waliosusia Filamu ya R. Kelly

 

Jay z na Lady Gaga ni mongoni mwa wanamuziki maarufu ambao walikataa kuonekana katika filamu inayoonyesha maisha halisi ya R.Kelly , mtayarishaji wa filamu hiyo ameeleza.

 

Makala hiyo ya ‘Surviving R Kelly’, ilizinduliwa jana nchini Marekani ikiwa imeangazia madai ya unyanyasaji wa kingono ambayo yamekuwepo dhidi yake kwa miongo kadhaa ambapo amekataa kuhusika na madai yote.

 

John Legend ni mwanamuziki pekee aliyekubali kuhojiwa kuhusu sakata hilo.

 

Mwezi Desemba 2018, mfululizo wa makala hiyo uliondolewa baada ya watu kuanza kupata simu za vitisho.

 

Muandaaji wa makala hiyo, Dream Hampton, alisema kuwa ilimwia vigumu kupata watu mashuhuri kushirikiana na R.Kelly ili iweze kuendelea.

 

“Tulimuomba Lady Gaga , Erykah Badu ,Celine Dion, Jay-Z, Dave Chappelle na wote walikuwa muhimu kwake,” lakini Hampton hakuamini kwa nini hawakumuunga mkono  wala jitihada zake.

 

John Legend ndiye mwanamuziki pekee ambaye alikubali kushiriki katika mfululizo wa makala hiyo ambapo ataonekana katika mfululizo wa mwisho wa filamu hiyo ambao ulirushwa Januari 5 mwaka huu.

 

“R Kelly amesababisha maumivu mengi kwa watu,” Hampton alisema.

 

Muimbaji huyo ambaye alikuwa anasifika kwa uimbaji, Hampton alimuita ‘shujaa’ licha ya kuwa jina hilo alilikataa.

 

“Kila mtu aliniambia nilipata ujasiri gani kuonekana katika makala hiyo, lakini mimi sikuona hatari yoyote,” John alisema.

Pamoja na kuwa mwanamuziki mwenye mafanikio makubwa katika historia ya muziki wa R&B, Kelly amekuwa akisakamwa kwa tuhuma za unyanyasaji wa ngono tangu mwaka 1990.

 

Makala hilo imefafanua uhusiano aliokuwa nao na mwanamuziki Aaliyah mwaka 1994, ambapo alimuoa Aliyah akiwa na umri wa miaka 15 wakati yeye akiwa na umri wa miaka 27.

 

Na badaye jarida la Vibe lilibaini kuwa Aaliyah alikuwa amedanganya umri wake katika cheti cha ndoa kwa kuandika kuwa ana umri wa miaka 18.  Ndoa hiyo ilifutwa mwezi Februari mwaka 1995.

 

Hivi karibuni mama yake Aliyah, Diane Houghton alitoa maoni yake alipohojiwa katika makala moja na kudai kuwa shutuma zote ni za uongo.

 

“Mume wangu alikuwa anasafiri na Aaliyah na alikuepo kwenye mahojiano yote na sehemu zote ambazo Aliyah alizuru kwa ajili ya muziki,” alisema.

 

Mfululizo wa filamu hiyo umemwonyesha mke wa zamani wa R Kelly aliyejulikana kama Andrea, ambaye pia alitoa madai ya unyanyasaji.

 

Mwaka 2018, R Kelly alizindua wimbo wenye dakika 19 unaoitwa ‘Admit’ ambao ulijibu madai kadhaa dhidi yake kuhusu ya ngono.

Toa comment