The House of Favourite Newspapers

Jazz Yatibua Bethidei Ya Lebron James

LeBron James.

UTAH Jazz iliumaliza mwaka 2017 kwa ushindi wa mbinde dhidi ya Cleveland Cavaliers katika siku ya kusherehekea kuzaliwa kwa mkali, LeBron James.

 

Donovan Mitchell aliiongoza timu yake ya Utah Jazz kupata ushindi wa pointi 104-101 akifunga pointi 29, rebaundi nne na asisti sita, Derick Favors alifunga pointi 19 na rebaundi sita, Ricky Rubio alikuwa na pointi 16, rebaundi 10 dabodabo, wakati fowadi Thabo Sefolosha alifunga pointi 10 na rebaundi 12.

 

LeBron James aliiongoza Cleveland kwa kufunga pointi 28, rebaundi nane na asisti sita, Jeff Green alikuwa na pointi 22 na rebaundi tano, Kevin Love alikuwa na pointi 20, rebaundi 10 dabodabo na Tristan Thompson alimaliza akiwa na pointi 11 na rebaundi tano.

 

Warriors yaichapa Griz-zlies

Stephen Curry alirejea katika kikosi cha kwanza cha Golden State Warriors kwa kufunga pointi 38 na kuisaidia Warriors kuichapa Memphis Grizzlies

141-128. Klay Thompson alikuwa na pointi 21 na asisti tano, na Kevin Durant alikuwa na pointi 20, rebaundi tano na asisti tisa.

Memphis iliongozwa na Marc Gasol aliyefunga pointi 27 na rebaundi sita, Tyreke Evans alikuwa na pointi 22 na asisti tisa, Kobi Simmons alikuwa na pointi 17 na JaMychal Green alimaliza mchezo akiwa na pointi 12 na rebaundi nane.

Sixers waichapa Nuggets

Philadelphia 76ers waliichapa Nuggets kwa pointi 107-102 huko Denver. Dario Saric akifunga pointi 20, rebaundi tisa na asisti sita, JJ Redick alifunga pointi 18, Robert Covington alikuwa na pointi 15, rebaundi 10 dabodabo, wakati Jerryd Bayless na Richaun Holmes wote walifunga pointi 14.

Jamal Murray aliiongoza Denver kwa pointi 31 na rebaundi nane, Nikola Jokic alikuwa na pointi 19, rebaundi 13 dabodabo, Gary Harris pointi 17 na Trey Lyles alimaliza akiwa na pointi 16 pamoja na rebaundi nane.

 

Hawks yaishushia kipigo Blazers

Nayo Atlanta Hawks iliichapa Portland Trail Blazers kwa pointi 104-89 kwa msaada mkubwa wa mlinzi Dennis Schroder aliyefunga pointi 22 na asisti nane, Marco Belinelli alikuwa na pointi 14, Ersan Ilyasova alikuwa na pointi 13 na rebaundi nane, wakati Taurean Prince alikamilisha usiku kwa pointi 12, rebaundi 10 dabodabo.

 

Portland iliongozwa na Shabazz Napier aliyefunga pointi 21, rebaundi nane na asisti sita, CJ McCollum alikuwa na pointi 18 na rebaundi nne, na fowadi wa Kinigeria, Al-Farouq Aminu alimaliza akiwa na pointi 10 na rebaundi tano.

Kwingineko

Pointi 14 na rebaundi 21 dabodabo kutoka kwa Andre Drummond ziliiwezesha Detroit Pistons kuichapa San Antonio Spurs 93- 79, Miami Heat iliichapa Orlando Magic 117-111 huku Tyler Johnson akifunga pointi 31, na pointi 30 za Kristaps Porzingis zilihitimisha ushindi wa New York Knicks wa 105- 103 dhidi ya New Orleans Pelicans.

Comments are closed.