Msanii wa Filamu za Bongo Movie, Jacob Steven maarufu kama JB ni miongoni mwa wasanii waliofanya kazi kwa karibu na marehemu Grace Mapunda.
Kupitia akaunti yake ya Instagram, JB ameandika:
“Tanzania imepoteza mmoja kati ya waigizaji bora kuwahi kutokea. Namshukuru sana Mungu kwa zawadi ya maisha yako… Nitamiss ucheshi wako, uigizaji wako mahiri lakini kubwa sauti yako.
Pumzika kwa amani rafiki yangu, pumzika Grace Mapunda, ilikuwa ni heshima kwangu na bahati kupata nafasi ya kuigiza nawe.