The House of Favourite Newspapers

JB Azua Gumzo Kupukutika Mwili

Jacob Stephen ‘JB’

MKALI wa sinema za Kibongo, Jacob Stephen ‘JB’ amezua gumzo la aina yake baada ya kutupia picha mpya mtandaoni inayomuonesha akiwa amepukutika mwili.

 

Akizungumza na Amani hivi karibuni, JB alisema siri ya kupungua kwake ni kupunguza kulakula hovyo na ndiyo maana ameweza kupungua kwa haraka huku mazoezi pia yakihusika.

 

“Mwanzo nilikuwa napenda sana kula vyakula, ndiyo maana nilikuwa na mwili mkubwa, lakini sasa hivi siendekezi tena kulakula hovyo, na ninahakikisha nafanya sana mazoezi, ndiyo maana unaona nimeweza kupungua kwa haraka,” alisema JB.

Stori: Memorise Richard, Amani.

Comments are closed.