JB: Kikwete anatuacha Pazuri

JB na KikweteStaa wa Bongo Movie, Jacob Steven JB akisalimiana na rais  Jakaya Kikwete.JB

MWANDISHI WETU

MKONGWE kwenye sanaa ya filamu Bongo, Jacob Stephen ‘JB’ amefunguka kuwa rais wa awamu ya nne anayemaliza muda wake, Jakaya Kikwete anaondoka madarakani akiwa ametoa msaada mkubwa sana katika sanaa.

Akizungumza na mwanahabari wetu hivi karibuni, JB alisema Rais Kikwete alikuwa akitoa msaada mkubwa sana kwa wasanii ikiwemo kushiriki katika masuala yao ambayo uwepo wake tu ulitosha kuifanya sanaa izidi kujulikana na kupiga hatua.

“Kikwete ametoa ushauri wa mawazo. Amekuwa akishirikiana nasi katika shida na raha. Kutuzungumza tu katika hadhara kwetu sisi ni jambo kubwa, tutamkumbuka kwa mengi sana,” alisema JB.

Loading...

Toa comment